Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
RAIS Dkt.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014 Toleo la 2023, ambayo inalenga kuleta mageuzi makubwa katika elimu nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma Msemaji Mkuu wa Serikali Greyson Msigwa amesema Sera hiyo itazinduliwa Januari 31 mwaka huu huku akisema mageuzi yaliyopo katika Sera hiyo ni pamoja na wanafunzi kufundishwa somo la Tehama, mafunzo ya ufundi stadi kuanzia elimu ya msingi na matumizi ya akili bandia(AI).
“Leo tumewaita kwa tukio lingine kubwa,kama mtakumvuka 2021 Rais Dkt. Samia alitangaza na kutoa malekezo akitaka Wizara yenye dhamana ya Elimu ifanye kazi kubwa ya kupitia Sera ya Elimu na lengo lake ilikuwa ni kuwa na sera ambayo itawanadaa wanafunzi kuwa Mahiri katika kukabiliana na changamoto na kujibu mahitaji ya Dunia ya sasa,
“Kwa maono ya Rais hakupendezwa na watoto wetu kuwa na madigrii lakini hawana ujuzi katika uzalishaji, matokeo yake wanapata shida katika maisha yao,kwa hiyo alitoa maelekezo na mara Moja Serikali tukaanza utekelezaji wa jambo hilo.”amesema Msigwa
Amefafanua kuwa,hatua iliyofikiwa katika utekelezaji kuelekea uzinduzi wa sera hiyo ni pamoja na kufanyika kwa mapitio ya iliyokiwa sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014 na kuwa Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014 Toleo la 2023 ambapo amesema sera iliyoandaliwa inalenga kuwa na wahitimu wenye maarifa,mwelekeo chanya maadili na ujuzi unaoakisi mahitaji ya kitaifa na kinataifa kuwezankushindana na kushiriki kikamilifu katika soko la ajira duniani
Amesema,mapitio hayo ya sera yanaakisi mahitaji ya kidunia ambayo yatatoa msukumo wa kuleta mageuzi katika sekta ya Elimu Ili kuzalisha rasilimaliwatu yenye maarifa,maadili na ujuzi utakaowawezesha wahitimu katika ngazi mbalimbali kujiajiri na kuajiri wengine na kuongeza uwezo katika soko la ajira duniani.
More Stories
Premium Active Tanzania yapunguza uhaba wa madawati Mlele
TARURA Kilindi kutumia bil.5.2 bajeti 2025/26
Madiwani Kilindi wapitisha bil.36.8 bajeti 2025/26