January 24, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Serikali yaja na mwarobaini wa changamoto ya Kivuko Magogoni – Kigamboni

Na Penina Malundo,Timesmajira

Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega amezindua mashirikiano kati ya Serikali na Sekta binafsi katika kituo cha Magogoni kwa kuzindua rasmi vivuko 2 ambavyo vitatoa huduma kwa wananchi, uwekezaji wa vivuko hivyo umefanywa na Azam Marine.

Akiongea wakati wa hafla hiyo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, RC Chalamila amesema tumefika hapa mara kadhaa tumeona namna watanzania wenzetu wanavyohangaika kwa kuwa bado Serikali ilikuwa haijatoa majawabu sahihi ya changamoto za vivuko.

Hivyo amemshukuru Rais Dkt Samia kwa kutafuta suluhu ya kilio cha wana Ilala, Wanakigamboni na watanzania kwa ujumla ambapo leo inajidhihirisha kupitia uzindua vivuko hivyo 2 Sea Tax 3 na Sea Tax 4 pamoja na kuweka mfumo wa kidijitali wa kukatisha Risiti na Kituo cha Kisasa cha Abilia kusubiria vivuko “Huo ni uwekezaji unaojibu changamoto za wananchi naipongeza sana Azam Group niwaombe muendelee kuwekeza na maeneo mengine” Amesema RC Chalamila .

Aidha RC Chalamila amesema TANROAD wana maeneo ya hifadhi za barabara ambayo ni vichaka, hivyo ameshauri maeneo hayo wapewe watu ambao wako serious na uwekezaji ambao utakuwa na tija na masilahi mapana kwa umma.

Sanjari na hilo vivuko hivyo vilivyozinfuliwa leo vinauwezo wa kubeba watu 240 kwa wakati mmoja kwa kasi ya dakika 5 hadi 6 hivyo uwekezaji huo unakwenda kuondoa kabisa changamoto ambayo wananchi wamekuwa wakiipata kwa kipindi kirefu.

Kwa upande wa Wakuu wa Wilaya ya Ilala na Kigamboni wamemshukuru, Rais kwa juhudi zake na maono katika kuleta ustawi kwa jamii hapa nchini hususani Wilaya ya Ilala ,Kigamboni na Mkoa kwa ujumla.