Na Joyce Kasiki,Dodoma
WAZIRI wa Afya Jenista Mhagama ameiagiza Bodi ya Wakurugenzi ya mFuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuona namna ya nzuri na ya haraka ya kutatua kwa haraka changamoto zinazooatikana kutokana na vifaa tiba
Waziri Mhagama ameyasema hayo. Jijini Dodoma wakati akizindua Bodi ya Sita ya WakurugenI ya Mfuko huo huku akisema lenyo la kufanya hivyo ni kuwafanya wanachama wasighadhibike.
“Wajumbe wa Bodi hii mnapaswa kuangalia namna bora itakayowezesha Mfuko kuhakikisha changazote zinazotokana na upatikanaji wa vifaa tiba, zinatatuliwa kwa haraka , kwa kushirikiana na wadau watoa huduma za afya ili wanachama wetu wasighadhibike kwa namna yoyote wanapohitaji huduma zilizo bora kutoka kwenye vituo vyetu vya kutolea huduma za afya”.amesema Mhagama
Aidha Mhagama amezungumzia mafanikio makubwa ya Mfuko huo ikiwemo ziada ya mapato huku akiitaka Bodi hiyo kuhakikisha mapato hayo yanatumika vizuri kulingana na thamani halisi ya fedha.
Katika hatua nyingine ameitaka Bodi hiyo kuhakikisha Sheria ya Bima ya Afya kwa wote inatekelezeka vyema na kukidhi natakiwa ya wananchi.
Vile vile ameiagiza Bodi hiyo kufanya kazi na sekta Binafsi Ili waendelee kusaidia Serikali katika sekta ya Afya na siyo kuwachukulia kama washindani.
“Sekta Binafsi imekuwa ikifanya kazi nzuri ya kutoa huduma za Afya kwa kushirikiana na Serikali hivyo natoa Rai kwenu ,mfanye kazi na sekta Binafsi kama Wadau Ili nchinisonge mbele zaidi kwa kutoa huduma Bora na nzuri za Afya na siyo kuwachukulia kama washindani wa Serikali.”amesiaitiza Mhagama
Aidha ameitaka Bodi hiyo kwa kushirikiana na wafanyakazi  kutoa  elimu ya kutosha kuhusu vifurushi walivyokubaliana na vinavyofanya kazi kwenye Bima ya Afya kwa wote lakini pia wazingatie misingi ya utawala Bora na kutomwonea haya Mtumishi yeyote anataka kuharibu taswira ya Mfuko.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Dkt.Irene Isaka alioneahwa kufutahishwa na uzinduzi wa Bodi hiyo huku akisema kwa kipindi Cha miezi sita tangu Bodi iliyomaliza muda wake ,Mfuko umekuwa ukiniendesha bila Bodi.
Hata hivyo ameelezea mafanikio ya Mfuko huo kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa mapato Kutoka nakisi ya shilingi bilioni 47 Hadi kuwa na ziada ya shilingi bilioni 111.
Vile vile amesema mafanikio mengine ni kuongeza wigo wa wanufaika wa Bima ya Afya kwa kusimamia usajili wa wanachama .
“Pamoja na mengi hayo ni mafanikio makubwa yaliyochangiwa na Bodi iliyomaliza muda wake,ingawa pia kulikuwa na changamoto mbalimbali.”alisema Dkt.Isaka
Amezitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa gharama za magonjwa yasiyoambukiza, Uhiari wa wananchi kjiunga kwenye mfuko wa bima ya afya na kukosekana kwa mfumo madhubuti wa rufaa ya wagonjwa nchini.
Awali Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Nchini (TIRA) , Dkt Baghayo Saqware alisema NHIF inachangia zaidi ya asilimia 80 katika sekta ya Bima na mifuko mingine inachangia chini ya asilimia 20.
Alisema,Mfuko wa Bima ya Afya kwa wote utakapoanza utazidi kushamirisha mchango wa sekta ya Bima.
Alitoa ombi kwa Waziri Mhagama ambapo alisema Wadau wa sekta ya Bima wanataka Sera ya Taifa ya Bima.
More Stories
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best
Waziri Mavunde:Benki Kuu yanunua tani 2.6 za Dhahabu nchini