January 19, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mkutano Mkuu maalumu CCM wapitisha Rais Samia ‘mitano tena’ Balozi Nchimbi aula

Na Agnes Alcardo na Joyce Kasiki. Timesmajira Online

SEKRETARIETI ya Halmashauri kuu Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), imetoka dokezo la pendekezo la kumteua Mwenyekiti wa CCM pia Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, awe mgombea wa Urais katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwaka huu 2025 kwa tiketi ya CCM huku Katibu Mkuu wa Chama hicho Balozi Emmanuel Nchimbi akiteuliwa kuwa Mgombea mwenza.

Pendekezo hilo limetolewa katika Mkutano Mkuu Maalum wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika leo Jijini Dodoma, ambapo wajumbe zaidi ya 1000 waliohidhuria kwenye mkutano huo, wameazimia kwa kauli moja kuwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, awe mgombea wa Urais katika uchaguzi Mkuu huo.

Aidha, Uamuzi huo wa mkutano mkuu umekuja kufuatia kazi nzuri walizozifanya katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, ambapo baadhi ya wajumbe waliuomba mkutano huo mkuu kutoa kauli moja kuwa Rais Samia na Rais Dkt Mwinyi kuwa wagombea Urais uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Ambapo, baada ya mapendekezo hayo kutoka kwa wajumbe wa mkutano huo, ilipelekea mwenyekiti mstaafu wa CCM Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete, kuwaambia wajumbe wa mkutano mkuu kuwa wajibu wa kupitisha azimio hilo ni la wajumbe wenyewe.

Hata hivyo, Dkt. kikwete ameshauri hatua za kisheria zizingatiwe ili kuondoa mgongano wa Kiserikali kulingana na taratibu za kuwapata wagombea, huku akisema kuwa chama kutangaza mapema mgombea wake ni jambo la kawaida.

Baada ya kutolewa kwa muongozo huo na Dkt. kikwete, ilipelekea Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia kuiagiza Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM chini ya Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Balozi Emmanuel Nchini kuiagiza kuandaa azimio la Mkutano mkuu la kuridhia uamuzi huo wa kumpimpitisha Mwenyekiti huyo Rais Dkt. Samia kugombea tena.Aidha, kwa upande mwingine, Dkt Kikwete ambaye ni mwenyekiti mstaafu wa CCM amesema ushiindi wa CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu hauna mjadala, hivyo CCM itashinda kutokana na mambo yake mazuri yaliyofanywa na Serikali zote mbili yanayogusa zaidi maisha ya watu.