Na Joyce Kasiki Timesmajira online,Dodoma
MBUNGE wa Mvumi ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Livingstone Lusinde ameibua shngwe kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) unaomalizika Leo jijini Dodoma kwa kuwaomba wajumbe hao wapitishe jina la Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea pekee wa kiti Cha Urais katika Uchaguzi Mkuu ujao kwa kipindi kingine Cha miaka mitano 2025-2030.
Aidha amewaomba wajumbe hao kupitisha jina la Rais wa Zanzibar anayemaliza muda wake Dkt.Hussein Ally Mwinyi kuwa mgombea pekee wa kiti Cha Urais kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar .
Akizungumza katika Mkutano Mkuu huo Maalum ,Lusinde amesema , hakuna sababu ya kuweka wagombea wengine kwa sababu wamefanya mambo makubwa katika Nchi hii hivyo Wana Kila sababu ya kupewa nafasi nyingine kwa kipindi Cha miaka mitano ijayo 2026-2030.
“Rais Samia ametekeleza Ilani ya CCM kwa zaidi ya asilimia 100 ,na mpaka hapo Rais hana deni isipokuwa sisi ndio tuna deni kwake,
“Kwa kutokana na hayo yote aliyotekeleza ikiwemo miradi mbalimbali katika Kila Kona ya Tanzania,naomba Wajumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu watoke sisi wajumbe tukadili suala hili kisha tutoke na azimio la viongozi wetu Hawa kuwa wagombea pekee katika Uchaguzi Mkuu ujao.”alisema Lusinde
Hoja hiyo ya Lusinde iliibua shangwe kwa wajumbe ikishiria kuungwa mkono kwa hoja hiyo ambapo baadhi ya wajumbe wallipata nafasi ya kuchangia na kuiunga mkono hiyo.
Naye Mwenyekiti wa CCM mkoa wa DODOMA ambaye pia ni mjumbe wa Mkutano huo Adam Kimbisa alisema,katika Uongozi wa Dkt.Samia ,Nchi nzima imezungukwa na miradi ikiwemo ya Afya,Elimu,maji ,miradi mkubwa ya kimkakati.
“Kwa sababu wajumbe wenye Chama tufanye jambo Moja ,tunalize kazi ,Mkutano huu uazimie kwamba Rais Dkt.Samia awe mgombea pekee kiti Cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Dkt Mwinyi awe mgombea kwa kiti Cha Urais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar”alisema Kimbisa
Mjumbe mwingine ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum mkoanwa Mwanza Mwasi Kamani alisema tayari wananchi katika maeneo mbalimbali na kufikia hatua hadi ya kutoa fedha zao kwa ajili ya kumuunga mkono Rais Dkt.Samia kuchukua fomu.
“Wapo hadi watoto wadogo wa shule ya msingi ambao walichangishana shilingi hamsini hamsini na mia mia zao walizopewa na wazazi wao na kupatikana shilingi 1,800 kwa ajili ya kumuunga mkono Dkt.Samia kuchukua fomu ya kugombea kiti Cha Urais ,naomba Wajumbe tukadili suala hili na tuazime viongozi wetu hawa wawe wagombea pekee .”alisisitiza Mwasi
More Stories
Wanafunzi 3000 wenye uhitaji wapatiwa vifaa vya shule
Mkutano Mkuu maalumu CCM wapitisha Rais Samia ‘mitano tena’ Balozi Nchimbi aula
Dkt.Kikwete:Ushindi wa CCM ni lazima