Na Penina Malundo,Timesmajira
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema Serikali itaendelea kuhakikisha inatoa msukumo kwa vijana kuhakikisha wanasoma na kupenda sayansi kwani ni mhimili wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam wakati akihitimisha la Tisa la Sayansi, Teknolojia, Ubunifu na Maonesho (STICE 2024), lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Prof. Mkenda amesema katika kuhakikisha masomo ya sayansi yanazidi kupendwa zaidi na wabunifu wanakuwa wengi,serikali itaendelea kuwekeza katika sekta ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu ili kuwawezesha vijana wa kitanzania kuona sekta hiyo inafursa kwao.
Amesema kuwa wakati umefika kwa wabunifu kuhakikisha kazi zao zinafika sokoni kwa ajili ya kutatua changamoto za kijamii, huku asisitiza kuongeza ubunifu zaidi katika kazi zao kwani sio vizuri kazi hizo za bunifu kujirudia kila mwaka
Prof.Mkenda amesema kuwa ni umuhimu wabunifu kutumia maarifa waliyopata katika kongamano hilo ili kuhakikisha sayansi na ubunifu havibaki kwenye maabara bali kubadilisha maisha ya watazania.
”Kongamano hili limefanyika kwa siku tatu ambalo limebeba kauli mbiu isemayo “Matumizi ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kwa Ustahimilivu wa tabianchi na Uchumi Shidani” limekuwa jukwaa muhimu kwa wataalamu wa sayansi, watafiti na wabunifu katika kubadilishana mawazo na kutafuta suluhisho za changamoto,”amesema na kuongeza
”Kongamano hili limepata fursa ya kuzindua mfuko wa samia ambao umelenga kusaidia wabunifu kwa kuwapatia mitaji ili kuendeleza bunifu zao ziweze kusaidia kuboresha maisha ya jamii na kukuza uchumi wa watanzania,”amesema.
Kwa Upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknlojia (COSTECH) Dkt. Amoss Nungu, amesema baadhi ya mapendekezo waliyoyatoa katika Kongamano hilo ni pamoja na kuifanya Teknolojia ya Ubunifu Kukuza Uchumi, kujenga uhusiano na wenye viwanda na kufanya mikutano ya pamoja ya eknolojia ya kukubaliana na mabadiliko ya Tabia nchi.
Amesema kuwa Kongamano hilo lilikuwa na malengo manne ambayo yamefikiwa kwa kiwango kikubwa ikiwemo kuwezesha usambazaji wa utumiaji wa matokeo ya utafiti na bidhaa za ubunifu.
Amesisitiza kuwa miongoni mwa malengo hayo ni kuhimiza ushirikiano kati ya watafiti, watenga sera na wadau wa sekta ya viwanda, kuhamasisha nafasi ya sayansi na ubunifu katika kushughulikia changamoto za Kitaifa na Kimataifa katika nyanja za ustamilivu, mabadiliko ya Tabia ya Nchi.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, Husna Sekiboko,amesema kuwa mapendekezo yaliyotolewa katika Kongamano hilo yanakwenda kufanyiwa na kazi kwa vitendo bungeni ili kuhakikisha yanakuwa na tija kwa manufaa ya Taifa
More Stories
Dkt. Kazungu atembelea miradi ya umeme Dar es Salaam
MSF ilivyojidhatiti kusaidia serikali katika utoaji wa huduma za afya
Prof.Muhongo awapongeza vijana 32 waliotembea kwa miguu kutoka Butiama hadi Mwanza