Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online. Dar
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, anatarajiwa kuzindua kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa wagombea wa chama hicho,Mkoa wa Mwanza,Novemba 20, 2024.Ambapo ataongoza viongozi na makada wa CCM,waliotumwa maeneo mbalimbali nchini kwa kazi hiyo.
Balozi Nchimbi, ambaye pia ni mlezi wa CCM Mkoa wa Mwanza, atazindua kampeni hizo katika mkutano wa hadhara utakaofanyika Uwanja wa Furahisha, wilayani Ilemela mkoani Mwanza.
Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, ambao ni walezi wa mikoa mingine, pamoja na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), wamepewa jukumu la kuzindua kampeni hizo katika mikoa yote 26 ya Tanzania Bara kwa tarehe hiyo hiyo.
Ambapo, Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa, Amos Makalla, atazindua kampeni ya Mkoa wa Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), John Mongella, atazindua kampeni Mkoa wa Mbeya, huku Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa,atazindua kampeni hiyo Mkoa wa Katavi.
Aidha, Viongozi wengine wa CCM waliopangiwa kuzindua kampeni ni pamoja na Issa Haji Gavu, Katibu wa NEC, Oganaizesheni, mkoani Geita, Rabia Himid Abdalla, Katibu wa NEC , Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI) mkoani Kilimanjaro na Dkt. Isdory Phillip Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mkoani Dodoma.
Pia, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa atazindua kampeni mkoani Kigoma, Tulia Ackson, Spika wa Bunge na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), mkoani Songwe na Hemed Abdulla Suleiman, Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar,atafungua mkoani Tanga.
Wengine ni Zuber Ali Maulidi, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, atafungua mkoani Singida, Komredi Mary Pius Chatanda, Mwenyekiti wa UWT Taifa, mkoani Arusha na Mizengo Pinda, Waziri Mkuu Mstaafu, atafungua mkoani Mtwara na Halima Mamuya, mkoani Njombe.
Katika kuendelea na zoezi hilo la ufunguzi wa Kampeni za Serikali za Mitaa, pia Nasir Ally Juma, atafungua zoezi hilo mkoani Tabora, Mohamed Aboud Mohamed, mkoani Iringa na Komredi Mohamed Ali Kawaida, Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, atafungua mkoani Morogoro, Fadhili Maganya, Mwenyekiti wa Wazazi Taifa, mkoani Simiyu.
Pia, Dkt. Dotto Mashaka Biteko, Naibu Waziri Mkuu, atafungua mkoani Mara, huku Hussen Bashe, akifungua mkoani Shinyanga na Livingstone Lusinde akifungua mkoani Manyara na wengine ni Ally Hapi, mkoani Kagera, Nape Nnauye, akifungua mkoani Rukwa, huku Zainab Shomari, akifungua mkoani Lindi na Salim Faraji Abri (Asasi), akifungua mkoani Ruvuma.
More Stories
DC Mgomi ataka wahitimu Jeshi la Akiba kuwa macho ya Serikali
Wadau wachangia vifaa Kariakoo
Dkt.Samia,aelekeza kuongezwa saa 24, zoezi la uokoaji Kariakoo