Na Penina Malundo,Timesmajira
RAIS Samia Suluhu Hassan ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam ,Jeshi la Polisi,Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili pamoja na Idara ya Menejimenti ya Maafa kufanya kila linalowezekana kufanikisha zoezi la uokoaji na tiba kwa majeruhi wa ajali ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa katika kata ya Kariakoo, Wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam.
Agizo hilo amelitoa leo baada ya kupokea taarifa ya ajali hiyo katika ukurasa wake wa Mtandao wa Kijamii amesema amesikitika kupokea taarifa ya ajali ya kuporomoka kwa jengo hilo la ghorofa katika Kata ya Kariakoo.
“Wakati zoezi hilo likiendelea na tukimuomba Mwenyezi Mungu awape pona ya haraka majeruhi, tuwaombee pia utulivu na subra ndugu,jamaa,marafiki na Watanzania wenzetu wanaotafuta riziki zao katika eneo hili muhimu kibiashara nchini ambao kwa namna mbalimbali wameathiriwa na ajali hii,”amesema Rais Samia.
More Stories
RC Mtambi awataka Maofisa kilimo kutoa elimu ya kilimo mseto
Rais Samia kuelekea nchini Brazil kushiriki mkutano wa G20
RC Chalamila awataka ndugu,Jamaa na marafiki kuwa wavumilivu zoezi la uokoaji likiendelea