September 21, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

DC Mpogolo awataka Wazazi kutoa elimu ya maadili kwa watoto

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

MKUU wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo amewataka Wazazi wilayani Ilala kushirikiana na viongozi wa chama katika kulea watoto katika maadili mema kwa ajili ya kuwajengea watoto msingi imara.

Mkuu wa wilaya Edward Mpogolo alisema hayo wakati wa semina kwa viongozi wa kata ya Tabata, Liwiti na Kimanga ngazi ya matawi na kata mkoni Dar Salaam.

Mkuu wa wilaya Edward Mpogolo alisema wazazi wa wilaya hiyo wakilea watoto katika misingi imara watamjenga mtoto katika maadili yanayofaa na kukubalika katika jamii .

“Viongozi tuwe wamoja kuwakemea vijana na wababa wanaoharibu watoto na tukatoe elimu kwa watoto ya mabadiliko na mahusiano ili kukwepa mimba za utotoni na maambukizi ya UKIMWI “alisema Mpogolo.

Aidha alisema takwimu zinaonyesha kuwa watoto chini ya miaka 17 wana maambukizi ya ugonjwa huo huku watoto wa kike wakiwa wanaongoza naomba viongozi wa chama mshirikiane na Wazazi walezi,katika kuwalea watoto kwenye malezi mema ili kujenga kizazi bora chenye maadili ambacho kitafuata mila na desturi za Taifa letu.

Katika hatua nyingine Mkuu wa wilaya Edward Mpogolo amewataka Wazazi kufatilia mienendo ya watoto hasa waliomaliza elimu ya msingi wasijiingize katika makundi hatarishi badala yake wajisomehe wakati wakisubiri matokeo yao ya kujiunga kidato cha kwanza.