*Ni ya Bei kama Mkaa ikihimiza wananchi kutumia gesi
Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline,Dar
KAMPUNI ya Puma Energy Tanzania kupitia PumaGas imezindua kampeni ya Bei kama Mkaa yenye faida nyingi yenye lengo la kuwahimiza wananchi kupika kwa nshati ya gesi ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Uzinduzi wa kampeni hiyo umefanyika jana Septemba jana, 2024 katika Viwanja vya Zakhem, Mbagala mkoani Dar es Salaam ambapo pia wananchi wameelimishwa kuhusu umuhimu wa kutumia nishati safi ya kupikia hususan ya PumaGas ambayo ni rafiki wa usafi na mazingira.
Akizungumza katika kampeni hiyo Meneja Masoko wa Puma Energy Tanzania, Lilian Kanora, alisema kampeni hiyo inalenga kuelimisha jamii na kuhimiza matumizi ya nishati safi kwani PumaGas inaokoa muda wa mama katika kupika, pia inatoa uhakika kwa mama kutoathirika kiafya kwa kuvuta moshi mwingi akiwa jikoni anapika.
Aliongeza kuwa kupika kwa nishati safi ya PumaGas kunasaidia ulinzi wa mazingira kwani hakutakuwa na sababu ya baba au mama kwenda kukata kuni porini na kuharibu mazingira.
Akieleza zaidi alisema kampeni hiyo inalenga kumhakikisha mwananchi kutumia fedha kidogo katika kununua nishati safi ukilinganisha na fedha anayotumia kununua
Mkaa.
“Nitawapa mfano kopo moja la mkaa ni Sh1000 hadi Sh.2000 na kwa familia inayopika milo mitatu kwa siku hii ni sawa na Sh.2000 hadi Sh.4000 kwa siku.
“Ukipiga hizi hesabu kwa mwezi ni zaidi ya Sh.60,000 wakati PugaGas kilo sita ni Sh.41000. Katika kampeni hii kutakuwa na punguzo la bei kqa mtungi wa kilo 15 awali mteja alikuwa akipata gesi na mtungi mpya kwa Sh.75000 ila kwa kipindi hiki kuna punguzo hadi Sh.66000.
“Mtungi wa kilo sita utapatikana kwa Sh.41000 tu na mtungi wa kilo 38 pamoja na gesi unapatikana kwa Sh.110,000,”amesema na kusisitiza Kampuni ya Puma Energy Tanzania imeweka mkakati maalum wa kuhakikisha wanashiriki kikamilifu jitihada za Rais Samia za kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034.
Alisisitiza kuwa Puma Energy Tanzania imekuwa na Serikali nyakati zote katika kampeni ya kuhamasisha nishati safi ya kupikia na wameshiriki vikao vyote vinavyozungumzia nishati hiyo na kinachofanyika katika kampeni ya Bei kama Mkaa faida Kibao ni kuonesha kwa vitendo dhamira yao ya kufanikisha mikakati ya nahati safi.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Mauzo PumaGas katika Kampuni ya Puma Energy Tanzania Jeffrey Nasser ametumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi wote kuunga mkono kampeni hiyo huku akishauri hasa wanaume kuwa sehemu ya kuleta mabadiliko kwa kuwezesha familia kutumia nishati safi ya kupikia ya PumaGas.
“Nitoe rai kwa wanaume ambao ndio baba wa familia,kuna msemo wa baba ni kichwa cha familia basi sasa wanaponunua mahitaji ya nyumbani yakiwemo ya chakula wahakikishe wananunua na nishati safi ya kupikia.
Akizungumza kuhusu mikakati ya kuhakikisha PumaGas inafika kwa wananchi wengi alisema baada ya kuanza na mkoa wa Dar es Salaam na Pwani wanaendelea kutanua wigo na siku za karibuni watafikisha huduma ya mitungi ya PumaGas Dodoma na maeneo mengine na kufafanua PumaGas inapatikana kwa mawakala wao pamoja na vituo vya mafuta vya Puma.
Wakati huo huo baadhi ya wananchi wa Mbagal na Pwani ambao wameshiriki katika uzinduzi wa kampeni hiyo wamesema wanatambua juhudi za Rais Samia katika kuhamasisha nishati safi ya kupikia hivyo nao wanamuunga mkono na wameshaachana na matumizi ya kuni na
mkaa.
More Stories
TAKUKURU,rafiki yanufaisha wananchi Mwanza
Mhandisi Samamba awasisitiza maafisa madini kusimamia usalama wa migoni msimu wa mvua
Wapinzani kutimkia CCM ishara ya ushindi Uchaguzi Serikali za Mitaa