Na Mwandishi wetu,Timesmajira
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, John Mongella, leo tarehe 05 Septemba 2024 ameanza ziara ya siku saba mkoani Shinyanga.
Lengo kuu la ziara hii ni kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2020-2024, kuimarisha uhai wa chama na kusikiliza changamoto zinazowakabili wananchi wa mkoa huo.
Mongella, ambaye ni mlezi wa chama mkoani Shinyanga, anatarajiwa kufanya mikutano ya ndani na hadhara, pamoja na vikao na watumishi wa chama na jumuiya zake.
Katika ziara hiyo, atatembelea maeneo ya Shinyanga Mjini, Shinyanga Vijijini, Kahama, Msalala, Kishapu, na Ushetu, ambapo atakutana na viongozi na wananchi kujadili namna bora ya kuimarisha utekelezaji wa sera za chama kwa maendeleo ya mkoa huo.
Kupitia ziara hii, Mongella anatarajiwa pia kuhamasisha wanachama wa CCM kushiriki kikamilifu katika shughuli za chama na kuwa mstari wa mbele katika kutatua kero zinazowakabili wananchi.
Ziara hii ni sehemu ya mikakati ya CCM ya kuhakikisha inaendelea kuwa karibu na wananchi na kujibu na kutatua kero zao kwa vitendo.
More Stories
Wagombea CHADEMA wakipewa ridhaa,watakuwa wawazi
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili