October 7, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Diwani Kimji achangia Mil. 1 Fomu ya Rais Samia

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

DIWANI wa Kata ya Ilala ambaye ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Wazazi CCM Taifa SAADY KHIMJI, amemkabidhi shilingi milioni 1 Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Zungu ,kwa ajili ya mchango wake wa Kumchangia fomu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kinyanganyiro cha Urais mwaka 2025.

Diwani Saady Kimji, alikabidhi pesa hizo kash.leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Ilala ambao ulikuwa ukielezea Utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM na kazi alizotekeleza ikiwemo miradi ya maendeleo katika ya Afya, Sekta ya Elimu na Miundombinu ya Barabara.

“Kata ya Ilala ,Jimbo la Ilala tuna mapenzi mema ya Rais wetu Mpendwa Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji wa Ilani ya chama vizuri ,Rais ametoa fedha nyingi za miradi ya maendeleo mimi Diwani wa Ilala nachangia Fomu ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan shilingi milioni 1 na kura zote za Ilala Elfu 12,500 tunampigia kura Dkt samia ili ashinde kwa kishindo 2025 “alisema Khimji

Diwani Kimji alisema katika uongozi wake utekelezaji wa ilani katika kata ya Ilala kwa ushirikiano wa Mbunge wake Mussa Zungu kata ya Ilala Upande wa sekta ya elimu Rais amejenga shule ya kisasa English Medium, shilingi milioni 300.9,shule ya sekondari Msimbazi shilingi milioni 340 ,Jengo la Utawala Msimbazi, ujenzi wa vyoo shule ya Msingi Ilala milioni 30,ukarabati wa vyumba 26 shule ya Msingi AMANA, pesa zimetolewa na Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu kutoka mfuko wa Jimbo .

Aidha alisema pia ugawaji wa Meza na Viti vya Walimu shule ya Msingi Karume milioni 10.6,na ukarabati unaendelea, shule ya Msingi MZIZIMA, Ilala, Kasuru,Mivinjeni wamepatiwa madawati 1422.

Alisema sekta ya afya kata ya Ilala kwa kushirikiana na wadau wamefanikiwa kujengewa Zahanati ya kisasa yenye hadhi kubwa ambayo ipo mtaa wa Mafuriko Bungoni kwa sasa huduma imeshaanza ilifunguliwa na Naibu Waziri Mkuu Doto Biteko.

Akizungumzia mafanikio katika miundombinu ya Barabara kazi Iliyofanywa kwa ushirikiano wa Mbunge wake Mussa Zungu alitaja baadhi ya Barabara zilizojengwa Ikiwemo ,Barabara ya Tukuyu, Mtaa Tanga,Mtwara, Moshi, Songea na Tunduru.

Wakati huo huo Diwani Saady Kimji aligawa Zawadi Maalum kwa Wenyeviti wake wa Serikali za mitaa kwa utendaji bora wa kazi na utekelezaji wa Ilani ya wakiongozwa Mwenyekiti Ally Mshauri,na HAJJI BECHINA