Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
NAIBU SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Zungu, ambaye ni Mbunge wa jimbo la Ilala amegiza maafisa Maendeleo kutoa mikopo ya Serikali kwa vikundi vya Jimbo la Ilala vyote bila kuwekewa vikwazo .
Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu ,alitoa agizo hilo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Ilala ambao umeandaliwa na Diwani Saady Kimji ,kwa ajili ya kuelezea utekelezaji wa Ilani ya chama.
“Maafisa maendeleo wetu wana changamoto katika mikopo ya ngazi ya Halmashauri ya asilimia kumi pesa nyingi za Serikali zimepotea kwa ajili ya Watendaji wasio na nidhamu nina agiza vikundi vyote jimbo la Ilala Wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu waweze kupewa mikopo wafurahie matunda ya Serikali yao mikopo hii inatolewa na Serikali aina riba”alisema Zungu,
Mbunge Zungu alisema, awali mikopo hiyo ya ngazi ya Halmashauri ilisimamishwa vikundi vilikuwa vinashindwa kukopa sasa hivi Rais Samia suluhu Hassan amerejesha ametaka maafisa maendeleo kufuata utaratibu ili iweze kuwafikia. Vikundi vyote vya wananchi bila kuweka changamoto ambazo zinafanywa na maafisa Maendeleo.
Aliagiza Maafisa maendeleo wote wa Jimbo Ilala kutoa ushirikiano kwa vikundi vitakavyoitaji mkopo bila kupewa vikwazo ili washindwe kukopa.
MNEC wa CCM Taifa SIMBA JUMA GADAF ambaye mgeni alikuwa mgeni rasmi, katika mkutano huo alisema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan, anafanya kazi kubwa usiku na mchana kuakikisha wananchi wake wanapata maendeleo kwa kutekeleza Ilani ya chama cha Mapinduzi katika sekta zote za Afya,Barabara na miundombinu ya Barabara.
Aidha MNEC Juma SIMBA Gadaf alisema wakati wa Uhai wake Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere, alikuwa anachukia Maadui watatu wakiwemo UJINGA, UMAKINI na MARADHI ambapo yote Dkt.Samia Suluhu Hassan ametekeleza kwa wananchi wake.
Pia alisema Chama cha Mapinduzi CCM kimefuta umasikini kwa kutoa fursa za mikopo ambapo alitumia fursa hiyo kuwataka watendaji kuondoa vikwazo vikundi vipate mikopo na kufanya biashara kujikwamua uchumi.
More Stories
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi
Mbunge Ndingo:CCM imejidhatiti kuwaletea maendeleo wananchi