November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

JUBI waomba Mikopo ya Serikali

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

JUMUIYA ya Uchumi JUBI wameiomba Serikali ya Dkt. Samia suluhu Hassan, awawezeshe taasisi yao JUBI kuwapa mikopo wanawake wa taasisi hiyo ambayo inashughulika na Wanawake na vijana pamoja na wananchi ili waweze kukuza uchumi kwa kuwawezesha mikopo ya asilimia kumi ambayo inatokewa ngazi ya Halmashauri.

Akizungumza katika Kongamano la Jumuiya ya Uchumi( JUBI DAY) inayoshughulika na wajasiriamali wa wilaya ya Ilala wa vikundi vinavyosimamiwa na taasisi ya JUBI VICOBA endelevu Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Mariam Kilunga alisema JUBI inashughukika na VICOBA endelevu hivyo Serikali ikiwapatia mikopo mikubwa watakopeshana kupitia VICOBA vyao ili wajikwamue kiuchumi JUBI iweze kusonga mbele.

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan, tunakuomba mikopo iweze kufikia taasisi yetu inatambulika kiserikali imesajiliwa sisi JUBI tuna miaka miwili toka kuanzishwa kwa taasisi yetu “alisema Mariam.

Mkurugenzi Mariam alisema JUBI ina unga mkono juhudi za Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, za kuwawezesha kiuchumi kwa ajili ya kukuza uchumi katika Tanzania ya viwanda.

Katibu wa Taasisi ya JUBI Mariam Joseph shayo, alisema Jumuiya ya uchumi bora ni Jumuiya isiyo ya Serikali inashughulika na wanawake, vijana na watoto pamoja na wananchi wote ambapo February 2023 ilisajiliwa rasmi mpaka kufikia February 2028 watafanya kazi Tanzania bara yote kwa mujibu wa Wizara.

Katibu Mariam alisema Kongamano hilo limewashirikisha wanachama wote wa vikundi pamoja na wadau mbalimbali ili kuweza kupeana elimu na kubadirisha uzoefu kwa ajiii ya kujiletea maendeleo ambapo kauli mbiu yao Jubi Mafanikio ni kazima.

Aidha alisema JUBI imeweza kuwaunganisha wanawake zaidi ya vikundi 25 wanawake, wanaume na Vijana, na watu wenye ulemavu katika vikundi vyao na kuwawezesha kielimu ya ujasiriamali, uwekezaji na matumizi ya pesa ili waweze kujiajiri na kupunguza umasikini katika familia na TAIFA .

“Kwa sasa Jumuiya yetu ya Uchumi JUBI inatoa mikopo kupitia vikundi vyao vya VICOBA na kuweza kutengeza akiba ya vikundi vyote na kutengeza faida kufikisha zaidi ya shilingi 56,759,000 pia wamefanikiwa kuanzisha mfuko wa Uwekezaji wa pamoja kwa ajili ya kufanya miradi ya kuwekeza fedha za kitanzania kiasi cha shilingi milioni 5,000,000/= kwa wanachama wa vikundi wa mfuko huo