November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Serikali yakifungia kiwanda cha kutengeneza pombe kali

Na Israel Mwaisaka,TimesMajira Online, Rukwa

Serikali imekifungia kiwanda cha kutengeza pombe kali aina ya banana kilichopo katika kata ya Ulumi wilayani Kalambo mkoani Rukwa kisha kumkamata mmiliki wa kiwanda hicho Nichoraus Shirima kutokana na kuanzisha kiwanda bila kuwa na vibali sambasamba na kutengeza pombe zinazo daiwa kuwa hatari kwa afya za watumiaji.

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Kalambo Shafi Mpenda akiwa ofisni kwake amesema wamekifungia Kiwanda hicho kutokana na kutokuwa na vigezo ikiwemo mazingira duni ya uzalishaji bidhaa,mazingira machafu,pamoja na ukosefu wa nyaraka muhimu za uanzishaji wa kiwanda kutoka kwenye mamlaka husika.

Licha ya hilo amesema baada ya kufanya ufuatiliji wa kina kwa kushirikina na vyombo vya usalama walibaini mwekezaji huyo kusambaza na kuzalisha bidhaa kinyume cha sheria na kusema halmashauri haina mgogoro na wawekezaji na badala yake inasisistiza wawekezaji kufuata sheria na taratibu za uwekezaji.

‘’kwa kushirikina na vyombo vya usalama baada ya kufika pale tulibaini uzalishaji wa kreti 300 za pombe na baada ya upekuzi wa kina tulibaini mwekezaji huyo anafanya biashara hiyo pasipo kufuata taratibu kwani hata Halmashauri tulikuwa hatuna taarifa zake kwani hata ukiangali kiwanda chake kilikuwa na uzalishaji mkubwa licha ya kuwa na muonekano mdogo’’ Alisema Mpenda.

Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha usafi na mazingira wilayani haumo Richard Manuma amesema wawekezaji hawanabudi kufuata sheria za usafi wa mazingira wakati wa uanzishaji viwanda ili kuepuka milipuko ya magonjwa.