Na Esther Macha, Timesmajira Online,Mbeya
JESHI la Polisi nchini limepiga marufuku maadhimisho ya Baraza la Vijana Taifa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Bavicha) baada ya kubaini kuwepo kwa viashiria vya uvunjifu wa amani.
Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini, Awadh Haji ametoa tamko hilo leo Jumapili Agosti ,11,2024 mkoani hapa sambamba na kutahadharisha wananchi kushiriki maadhimisho hayo yalitarajiwa kufanyika kesho Agosti 12,2024 katika viwanja vya Ruanda nzovwe jijini hapa.
Haji amesema wamefikia hatua hiyo kutokana na kauli zinazotamkwa na viongozi zikieleza kwamba wanakwenda kuamua hatma ya Taifa la Tanzania wako serious kama vijana wa Kenya walivyojitambua na kuacha uteja na serikali.
Pia ameonya watu walionza safari kutoka mikoa mbalimbali nchini kuja mkoani Mbeya kushiriki maadhimisho kutodhubutu kwa kile alichoeleza kutoa maelekezo kwa makamanda wa Polisi nchini.
Miongoni mwa maelekezo ni kuwataka kufanya ukaguzi wa vyombo vya moto na endapo wakibaini kuna watu wenye viashiria vya kuja kushiriki wachukuliwe hatua za kusheria .
More Stories
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa
NLD kipo tayari kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa