Mwenyekiti Wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe.Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele, akizungumza wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Waratibu wa Uandikishaji wa mkoa, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa halmashauri yaliyoanza leo tarehe 10 hadi 11 Agosti, 2024 Mkoani Mkoani Mwanza.

Washiriki wa Mafunzo yaliyotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kwa Watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mkoani Mwanza, wakila kiapo cha kujitoa uanachama wa chama cha siasa na kutunza siri wakati wa kutekeleza majukumu yao. Mafunzo hayo yameanza leo tarehe 10 Agosti, 2024 na yamehusisha Mratibu wa Mkoa wa Uboreshaji wa Daftari, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Uchaguzi, Maafisa TEHAMA na Maafisa Ugavi wa halmashauri zote za mkoa wa Shinyanga. Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Mkoani Mwanza na Shinyanga utafanyika kuanzia tarehe 21 hadi 27, Agosti, 2024 ambapo vituo vitafunguliwa saa 02:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhani akifafanua jambo.
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Asina Omari akifafanua jambo wakati wa mafunzo hayo.
Mmoja wa wakufunzi kutoka Idara ya TEHAMA na DAFTARI akitoa somo la ujazaji wa fomu mbalimbali zinazotumika wakati wa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Mmoja wa wakufunzi kutoka Idara ya TEHAMA na DAFTARI akitoa somo la ujazaji wa fomu mbalimbali zinazotumika wakati wa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Washiriki wa Mafunzo wakifanya mafunzo kwa vitendo.
Washiriki waklifuatilia mada wakati wa mafunzo.
**************
Na Mwandishi wetu, Mwanza
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetaka
watendaji wakati wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura Mkoani Mwanza
na Shinyanga kuhakikisha wanatunza vifaa vya uandikishaji ili vikaweze kutumika
maeneo mengine nchini.Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa Jacobs Mwambegele wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Waratibu wa Uandikishaji wa mkoa, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa halmashauri yaliyoanza leo tarehe 10 hadi 11 Agosti, 2024 Mkoani Mkoani Mwanza.
Mafunzo kama hayo pia yamefunguliwa Mkoani Shinyanga na Makamu Mwenyekiti wa Tume, Jaji wa Rufaa(Mstaafu) Mbarouk Salim Mbarouk leo mkoani humo.
“Kwa kusisitiza, ni muhimu kutekeleza majukumu yenu kwa umakini katika kila eneo ikiwemo utunzaji wa vifaa vya uandikishaji hasa ikizingatiwa kuwa, vifaa hivi vimenunuliwa kwa gharama kubwa sana na vinatarajiwa kutumika katika maeneo mengine ya uandikishaji nchini,” alisema Jaji Mwambegele.
Amesema kutokuwa makini katika utunzaji wa vifaa hivi kutapelekea athari kubwa katika ukamilishaji wa zoezi hili muhimu na amewataka kuzingatia maelekezo yote yatakayotolewa na Tume ili muweze kuyafanyia kazi wakati zoezi litakapokuwa limeanza.
Aidha, Jaji Mwambegele amesema matokeo bora ya zoezi hili yanategemea uwepo wa ushirikiano mkubwa kati ya watendaji wote wa uboreshaji, serikali, vyama vya siasa na wadau wengine wa uchaguzi.
“Ninawasihi muwe na ushirikiano mzuri na wa karibu na Tume wakati wote mtakapokuwa mnatekeleza majukumu yenu na ikiwa mnahitaji ufafanuzi au maelekezo yeyote, msisite kuwasiliana na Tume,” alisema Jaji Mwambegele
Mapema kabla ya kuanza mafunzo hayo, washiriki walikua kiapo cha kujitoa uanachama na kile cha kutunza siri mbele ya Hakimu Mkazi wa Mwandamizi wa Wilaya Ilemela, Christian Mwalimu.
Mafunzo hayo yanahusisha namna ya ujazaji wa fomu pamoja na kutumia mfumo wa kuandikisha wapiga kura (Voters Registration System – VRS) ili waweze kupata uelewa wa pamoja utakaowapa fursa ya kutumia kwa ufasaha mfumo huo pamoja na vifaa vingine vya kuandikisha wapiga kura.
“Mafunzo haya, yanawajengea umahiri wa kuwafundisha Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Kata kisha nao watatoa mafunzo hayo kwa Waendeshaji wa Vifaa vya Bayometriki na Waandishi Wasaidizi ambao ndio watahusika na uandikishaji wa wapiga kura vituoni,” alisema Jaji Mwambegele.
Aidha, Maafisa TEHAMA watapatiwa mafunzo maalum ya jinsi ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiufundi (Troubleshooting) endapo zitajitokeza wakati wa zoezi la uandikishaji wa wapiga kura vituoni.
Katika hatua nyingine, Jaji Mwambegele amewaambia watendaji hao kuwa wakati wa uboreshaji wa Daftari mawakala wa vyama vya siasa wataruhusiwa kuwepo katika vituo vya kuandikisha wapiga kura jambo ambalo litasaidia kuleta uwazi katika zoezi zima lakini pia mawakala hao watasaidia kutambua waombaji wa eneo husika hivyo kupunguza kutokea kwa vurugu zisizokuwa za lazima.
Jaji Mwambegele alitoa angalizo kwa mawakala hao kutoka vyama vya siasa kuwa hawaruhusiwi kuwaingilia watendaji wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yao vituoni.
Tume tayari imeanza zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambapo mzunguko wa kwanza ulianza kwa mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora kuanzia Julai 20 hadi 26,2024 na mzunguko wa pili unaendelea katika mikoa ya Kagera na Geita ambao ulianza Agosti 5 hadi 11 mwaka huu, na kauli mbiu ya uboreshaji ni “Kujiandikisha Kuwa Mpiga Kura Ni Msingi Wa Uchaguzi Bora”
More Stories
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili
ACT-Wazalendo,waitaka Polisi kutobeba chama kimoja