Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji na Mbunge wa Jimbo la Ubungo Prof. Kitila Mkumbo amepiga marufuku askari mgambo wanaonyanyasa wafanyabiashara katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo wa Kata ya Makuburi.
Prof. Kitila akiwa katika Mkutano wa hadhara Makuburi Kibangu Dar es Salaam baadhi ya wafanyabiashara wamewasilisha kero ya kufukuzwa kwenye maeneo yao na askari mgambo hali iliyolazimu kutolewa kwa marufuku hiyo.
“Haiwezekani Wananchi wanahangaika kujitafutia riziki mnawasumbua, hii haikubaliki, mnadhani watapata wapi Chakula, kuanzia sasa kwenye maeneo yote nchini, ni marufuku kwa askari mgambo kuwasumbua wafanyabiashara” Prof. Kitila Mkumbo.
Amesema Serikali inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan imekuwa ikiwajali Watanzania na kuthamini utu wao huku ikihakikisha inaweka Mazingira rafiki ya ufanyaji kazi na biashara.
Kabla ya kufanya mkutano na wananchi Prof. Kitila amekutana na vikundi mbalimbali vya akina Mama na Vijana kwenye Kata ya Makuburi ambao wameipongeza Serikali ya awamu ya sita Kwa kuendelea kuwaletea maendeleo.
Miongoni mwa vikundi vilivyotembelewa ni kikundi cha Mama Lishe EPZA ambapo Prof. Kitila Mkumbo ameahidi kuwajengea vibanda katika eneo lao la kufanyia biashara.
More Stories
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa
NLD kipo tayari kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa