Na Bakari Lulela, Timesmajira Online DSM
KITUO cha Sheria na haki za binadamu ( LHRC) kimefanya uchambuzi wa muswada wa mabadiliko ya Sheria namba 2,2024 ambao unalenga kurekebisha Sheria ya uhamiaji sura namba 54 pamoja na Sheria ya ardhi, Sheria pendekezwa ( No. 2) act, 2024 imeweka mapendekezo ya kubadili vifungu vya Sheria za uhamiaji na ardhi sura namba 54 na sura namba 113 mtawalia.
Akitoa tamko Hilo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es salaam, mkurugenzi mtendaji wa kituo cha Sheria na haki za binadamu Dkt. Anna Henga amesema msingi wa tamko Hilo ni kutoka kwenye katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania 1977.
“Inaweka uhuru wa kutoa maoni na haki ya ushiriki wa wananchi katika mambo yenye maslahi na maisha yao ikiwemo mchakato wa kutunga Sheria kwa kupitia kujadili na kutoa maoni kwa njia mbalimbali kupitia vyombo vya habari, kuwasilisha maoni yao kwa wawakilishi wao au kushiriki mbele ya kamati ya bunge husika,” amesema Henga
Aidha Henga amesema kuwa lengo la tamko Hilo ni kuisaidia jamii kutambua na kujua muswada huo pamoja na maoni ya ujumla ya LHRC ili kurahisisha ushiriki wao katika utunzi wa Sheria, pia kutoa mapendekezo kwa serikali na wabunge wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Hata hivyo muswada huo unapendekeza kurekebisha vifungu 17 vya Sheria ya uhamiaji ambavyo baadhi ya vifungu vinalenga kuanzisha ‘hadhi maalum ya uraia’ baada ya kupitia muswada huo ambapo LHRC imebaini kuwa muswada huo ni kuleta suluhisho na muafaka ya muda mrefu kutoka kwa jamii ya diaspora juu ya haki ya uraia, haki ya kumiliki Mali, haki ya utambulisho wa asili kwa jamii za watu wenye asili ya Tanzania.
Mkuu huyo amesema kuwa miongoni mwa changamoto zilizobainiwa ni pamoja na kusitishwa kwa hadhi maalum kwa kosa la kutoa kauli isiyo na utii kwa jamhuri ya muungano wa Tanzania ambapo muswada huo inaweka MAMLAKA makubwa kwa Kamishna mkuu wa uhamiaji kusitishwa hadhi maalum ambayo ina athari ya kufutwa kwa haki ya kumiliki ardhi.
Ameeleza kuwa kifungu hicho kinaathiri uhuru wa kujieleza kwa hofu ya kusitishiwa hadhi maalum ikiwa kauli hiyo itatafsiriwa na Kamishna kuwa Haina utii kwa jamhuri ya muungano wa Tanzania.Amesema kifungu hicho kinakinzana na ibara ya 18 ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania,1977 inayoweka uhuru wa kujieleza ambapo madhara yake ni kuzuia watu wote walipewa hadhi kutoa maoni kwani kutafsiriwa kuwa yanakosoa serikali.
Changamoto nyingine ni kusitishwa kwa hadhi maalum kwa kosa la utovu wa maadili inaweza kubatilishwa Kamishna ataona si vyema kwa manufaa ya umma kuendelea kushikilia hadhi LHRC inaona kuwa maamuzi hayo ya naweza kutafsiriwa kwa namna mbalimbali ambavyo inamuweka diaspora katika hatari.
Aliendelea kusema kipimo cha maadili mema kama moja ya sifa kupewa hadhi maalum ambapo kifungu cha 36 cha muswada inaweka sifa za kupewa hadhi maalum mwombaji anatakiwa kuonyesha ana maadili mema kifungu hiki kinachangamoto ya tafsiri na utekelezaji wake Sheria haijaweka mchakato wa utoaji wa hadhi maalum badala yake MAMLAKA ya utoaji wa hadhi yapo kwa Kamishna mkuu wa uhamiaji.
Amesema kutumika kwa vigezo tofauti vya kutoa hadhi maalum ibara ya 22 ya muswada unapendekeza kuongeza kipya cha 36B ambacho kinampa Kamishna mkuu wa uhamiaji MAMLAKA ya kutoa hadhi maalum kwa kuzingatia mazingira maalum pale atakapoona inafaa ikiwa mtu huyo ana kipaji au ujuzi changamoto ya kifungu hiki ni baadhi ya watu kupewa mwanya wa kupewa hadhi chini ya kifungu cha 36A kinachoweka sharti la mtu huyo kiheshimu maadili ya kitaifa, Mila, desturi na utamaduni
Kipengele hiki kinapaswa kurekebishwa ili kuepuka tafsiri na matumizi ya kibaguzi ambapo hali hii inaweza kusababisha kesi za kikatiba mbele ya mahakama kuu kwa mujibu wa ibara ya 26 na 30 (3) ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania 1977.Kuendelea kutumia kifungu kilichobatilishwa na mahakama kuu ya Tanzania ambapo kifungu 23 kinapendekeza kurekebisha kifungu cha 37 ya Sheria kinachoweka utaratibu wa kukata rufaa kwa waziri mwenye dhamana.
More Stories
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa
NLD kipo tayari kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa