November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Vituo vinavyojiendesha TMA kutoa utabiri wa uhakika

Na Joyce Kasiki,Dodoma

MENEJA Huduma za Hali ya Hewa,Kilimo Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Isack Yonah amesema ,TMA imeshiriki maonesho ya wakulima na wafugaji kwani ni mdau mkubwa wa sekta ya kilimo.

Aidha TMA imeboredha huduma zake za hali ya hewa kwa kuweka vituo vya hali ya hewa vinavyojiendesha vyenyewe ili kutoa itabidi wa uhakika.

Akizungumza na wandishi wa habari kwenye banda la TMA viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma amesema, lengo la kushiriki maonenesho hayo ni kuelimisha wananchi kwa huduma wanazozitoa kwa sekta ya Kilimo na sehemu nyingine za uchumi kwa sababu TMA ni sekta mtambo unahudumia watu na maeneo mbalimbali .

“Kwa hiyo tumekuja hapa ili kujibu baadhi ya maswali yanayoulizwa na wananchi lakini pia watupe mahitaji yao ili kilimo chao kiweze kuwa bora kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa ambayo huathiri mazao ya wakulima,

“Kwa hiyo Mamlaka na Serikali kwa ujumla inawekeza sana kwa vifaa na mitambo ili kuhakikisha kwamba utabiri unatolewa ni wa uhakika .”amesema Yonah

Ameongeza kuwa “Kwa hiyo sisi TMA upande wa kilimo tuna vituo vya hali ya hewa kwenye sekta ya kilimo ambayo kwenye vituo vyote vya utafiti wa kilimo TARI na TACRI tuna vituo vya hali ya hewa ambavyo kazi yake ni kutoa taarifa za hali ya hewa kwa ajili ya utafiti wa mazao yanayoweza kuendana na kilimo cha sasa na mabadiliko ya hali ya hewa.”

Amesema katika kuboresha huduma zao wameweka vituo vinavyojiendesha vyenyewe na kuachana na ile Teknolojia ile ya zamani ambayo mtu anaenda anaangalia na kutoa utafiti ambao pengine anaweza kukosea kusoma,au wakapita wanyama wakaharibu.

Yonah amesema,Vituo hivyo vinavyojiendesha vyenyewe inachukua takwimu na kuziongoza kwenye mifumo ya utabiri na kupata utabiri ambao ni bora zaidi na hivyo kusaidia kilimo na wakulima kwa ujumla