November 21, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TPHPA inavyochangia utoshelevu wa chakula nchini

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

MKURUGENZI  Mkuu wa Mamlaka ya Mimea na Viuatilifu nchini (TPHPA) , Profesa Joseph Ndunguru amesema ,Mamlaka hiyo imekuwa ikitekeleza shughuli zake kwa kuzingatia vipaumbele vya Wizara ya Kilimo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha nchi inakuwa na utoshelevu wa chakula.

Profesa  Ndunguru ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya wakulima na wafugaji jijini Dodoma.

Amesema,Mamlaka hiyo imefanya kazi kubwa ya kudhibiti kweleakeelea waliokuwa wakishambulia mazao nchi na hivyo kuchangia utoshelevu wa chakula nchini.

“Mamlaka ya Mimea na Viuatilifu nchini (TPHPA), ina mchango mkubwa katika kuwa na utoshelevu wa chakula nchini  kutokana na jitihada inayofanya ya kudhibiti visumbufu vya mazao vikiwemo kweleakwelea na visumbufu vingine.”amesema Profesa Ndunguru na kuongeza kuwa

“Katika  siku za hivi karibuni TPHPA imefanikiwa  kudhibiti ndege aina ya kweleakwelea ambao walikuwa wakishambulia mashamba makubwa ya mpunga.”

Amesema ,hatua hiyo imekuwa niliongeza tija ya uzalishaji katika sekta ya kilimo kutokana na Udhibiti wa visumbufu vya mazao shambani.

Vile vile amesema, katika kuhakikisha mazao yanayopatikana yanakuwa na soko,  mamlaka imeandaa taarifa ambayo inasaidia kufunguka kwa masoko katika nchi 15 huku akisema ,hivi karibuni mabalozi watakabidhiwa taarifa hizo.

Aidha amesema,utekelezaji wa majukumu hayo yote ya Mamlaka hiyo  kwa namna moja ama nyingine unasaidia katika ukuaji wa Pato lanTaifa nchini.