November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wananchi fikeni Baraza la ukunga kutoa malalamiko

Na Joyce Kasiki,Dodoma

BARAZA la Uuguzi na Ukunga Tanzania,limetoa rai kwa wananchi kufika kwenye Baraza hilo iwapo atapata changamoto yoyote wakati anapatiwa huduma za afya.

Aidha mgonjwa anatakiwa kufika kwenye Baraza hilo akiwa ameshaanzia ngazi ya chini ambapo akiona hajaridhi ndipo afike katika baraza hilo kuwasilisha changamoto zake.

Akizungumza na waandiahi wa habari katika.maonesho ya wakulima na wafugaji katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma,Ofisa Habari na Mawasiliano wa Baraza hilo Ndimnyake Mwakapiso amesema,kumekuwa na changamoto wanapata wagonjwa lakini hawajui malalamiko yao wayapeleke wapi.

“Kama kuna mgonjwa ambaye hakutendewa sawasawa , kuna ngazi ya malalamiko kuanzia kituo cha afya hadi mkoa na kama hajaridhika anaweza kwenda Baraza la Ukunga na uuguzi kupeleka malalamiko,”.amesema Afisa habati huyo

Amesema mara nyingi kupitia maonesho mbalimbali wamekuwa wakielimisha wananchi kupitia njia mbalimbali ili wananchi wajue baraza hilo ni chombo chao cha kufikishia kero wanapokuwa na shida.

Amesema baraza hilo linasimamia taaluma ya uuguzi na ukunga kuhakikisha kundi hilo kubwa la watoa huduma kwa kufuata misingi, taratibu, miiko, kanuni na sheria.

“Yapo majukumu mengi ambayo baraza linafanya, moja kati ya majukumu makuu ni kumshauri waziri wa Afya kuruhusu masuala yote ya sera ya uuguzi na ukunga, kama kuna marekebisho, kuna kitu cha kuongeza,” amesema.

Amesema baraza hilo ni muhimu kwa kuwa chuo hakiwezi kutoa taaluma ya uuguzi au ukunga bila kusajiliwa na baraza hilo.

Katika hatua nyingine, amesema mwaka jana wa fedha kulikuwa na mashauri takribani 26 ambayo waliyapokea, hivyo wapo wahusika waliopewa onyo na wengine kusimamishwa kazi miaka miwili.