Foundation for Civil Society (FCS) na Baraza la Ushauri la watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Tanzania (TCRA CCC) zimetiliana saini ya makubaliano ya miaka mitatu yenye lengo la kuimarisha juhudi za kulinda haki za watumiaji wa Huduma katika sekta ya Mawasiliano nchini Tanzania.
Akizungumza na Waandishi wa habari leo Agost 6 ,2024 Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Bw.Justice Rutenge amesema kwamba huo unatambua umuhimu wa kuwalinda watumiaji dhidi ya mbinu za kibiashara zisizo za haki katika soko.
” Ubia huu unalengo la kuhakikisha haki na uwajibikaji katika kutoa Huduma kwa watumiaji na kiwawezesha kufanya maamuzi sahihi wanaponunua na kutumia bidhaa na Huduma za kulinda haki za watumiaji (Consumer Protection)unachangia maendeleo ya masoko na ukuaji wa biashara” amesema Rutenge.
Nakuongeza kuwa” Biashara zinazoheshimu sera za kulinda watumiaji na kuwapa wateja wao kipaumbele hujijengea hadhi na kuziweka katika nafasi nzuri kiushindani,hii huzihakikishia biashara hizo uwepo wa wateja wa uhakika na kuweka meingi mzuri wa ukuaji.
Aidha ameendelea kufafanua kuwa katika soko la sasa lenye mabadiliko ya haraka,uadilifu katika biashara unategemea kwa kiasi kikubwa kulinda haki za watumiaji dhidi ya mbinu zisizo za haki na udanganyifu katika biashara.
Bw.Rutenge amesema kwamba Wafanyabiashara Wana nafasi muhimu katika kuhakikisha uwazi na usahihi katika shughuli zao,hivyo FCS na TCRA CCC zimeunganisha nguvu katika kubuni na kutekeleza mradi unaolenga kulinda haki za watumiaji wa bidhaa na Huduma za Mawasiliano nchini Tanzania.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa TCRA CCC ,Bi.Mary Shao Msuya amesema kwamba Baraza Hilo limeanzishwa kwa lengo la Kuhakikisha maslahi ya watumiaji wa Huduma za Mawasiliano za TEHAMa,Huduma za Utangazaji,Huduma za Posta,na Virus Hi na Vipeto.
Amesema kuwa huduma za Mawasiliano nchini zinaongezeka kitokana na ukuaji wa kasi wa teknolojia kwa mujibu wa takwimu za TCRA ,kufikia June,2024 kuna kadi za simu milioni 76.6,watumiaji wa internet milioni 39.3,akaunti za pesa mtandao milioni 55.7, ambapo idadi hiyo itaendelea kuongezeka na Huduma mpya zitaongezeka kutokana na kukua kwa teknolojia ya kidijitali.
“Ukuaji huu wa teknolojia ni muhimu hasa wakati nchi yetu imejukita kwenye uchumi wa kidigitali ,Mawasiliano yanaweza kufikisha taarifa kwa wakati ,uendeshaji wa shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo Biashara,uzalishaji ,elimu,afya na upatikanaji wa Huduma jumuishi za kifedha.
More Stories
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili
ACT-Wazalendo,waitaka Polisi kutobeba chama kimoja
Gavu aanika miradi iliyotekelezwa na Serikali ya awamu ya sita Geita