Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO), limewataka wananchi kutoogopa kutumia umeme katika matumizi mbalimbali ikiwemo ya kupikia kwa kuwa vifaa vinavyotumia umeme vimeboreshwa hivyo hutumia umeme mdogo.
Meneja Masoko wa shirika hilo, Sylivester Matiku ameeleza hayo katika maonesho ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi yanayoendelea katika Viwanja vya Nziguni, Dodoma.
Matiku amesema , “Vifaa vinavyotumia umeme vimeboreshwa kwa hivyo kuwezesha kutumika kwa umeme wa gharama ndogo katika matumizi mbalimbali tofauti na ilivyokuwa zamani.
“Hivyo tupo hapa nanenane kuwaelimisha wananchi mambo mbalimbali pamoja na kuwaambia, wasione kutumia umeme kupikia ni ghali kama ilivyokuwa zamani yote haya ni kwa kuwa teknolojia imeboreshwa,” amesema.
Amesema katika matumizi bora ya vifaa vya umeme kuna vifaa vya kutumia umeme mdogo kama taa, zinaboreshwa hivi sasa.
“Tunayo majiko, friji, zinazotumia umeme kidogo mwisho wa siku ukiona umeme halisi uliotumia unakua umeme kidogo,” amesema.
Amewataka wananchi kutokupata hofu katika kutumia umeme kwa kuwa teknolojia zimekuwa zikiboreshwa.
Katika hatua nyingine ameelezea uboreshaji wa mita za umeme unaoendelea hivi sasa nchi nzima, na hivi sasa unafanyika mkoa wa Dar es Salaam.
Amesema hapo nyuma Tanesco walikuwa na mita ambazo hivi sasa zinaboreshwa katika teknolojia mpya.
“Itakapofikia Novemba 24 mwaka huu tutahakikisha watu wote wameingia kwenye ubireshaji wa mita.
“Uboreshaji wa mita kutakuwa na token namba moja hadi mbili itahusisha uboreshaji wa mita, token namba tatu ndio kuingiza unit za umeme ” amesema.
Kwa upande wake. Ofisa Mkuu Afya na Usalama kazini kutoka Tanesco, Nelson Mnyanyi amesema lengo lao ni kuhakikisha hakuna mkulima ama mfugaji anayepata ajali.
Amesema kwenye maonyesho hayo wapo kwa ajili ya kutoa elimu kwa wakulima na wafugaji kuhusu matumizi bora ya umee wawapo kwenye shughuli zao za kila siku.
Ametoa mfano kuwa wakulima wanapochoma moto wanapaswa kuwa makini ili wasiunguze nguzo za umeme, wafugaji nao wanapochungawasindandie nguzo za umeme kuepuka ajali zinazoweza kutokea.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi