November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kampeni ya kisheria ya mama Samia yawafikia zaidi ya 4,000

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

KAMPENI ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia mpaka sasa imehudumia wananchi zaidi ya 4,000 waliokuwa na changamoto mbalimbali za kisheria katika jamii katika mikoa saba hapa nchini.

Kaimu Mkurugenzi Kitengo cha Huduma cha Msaada Kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Ester Msambazi amesema hayo katika maonesho hayo yanayoendelea jijini Dodoma huku akisema tangu Agosti Mosi, 2024 maonesho hayo yalipoanza, kampeni hiyo imefanikiwa kusikiliza migogoro 26.

Msambazi ambaye pia ni Msajili wa Mashirika yanayotoa huduma ya msaada wa kisheria, ametaja huduma zinazotolewa kuwa ni ushauri wa kisheria pamoja na kuwaandalia wananchi nyaraka za kisheria ili waweze kuwasilisha mahakamani.

Pia kutoa elimu kwa makundi yanayowatembelea wakiwemo wanafunzi, wanawake wa vikundi vya kiuchumi, kusikiliza migogoro ya mtu mmoja mmoja ambapo toka maonesho yameanza wameshasikiliza migogoro 26.

“Migogoro hiyo inahusu ardhi, mirathi, ndoa, matunzo ya watoto na migogoro mingine. Kwa hiyo tunatoa rai kwa wananchi wa Dodoma na mikoa jirani wafike katika banda wapate elimu ya msaada wa kisheria,” amesema.

Amesema huduma hizo za kisheria zinagharimiwa na Rais Samia Suluhu Hassan