November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Askofu amshauri Samia kuhusu taasisi za fedha  

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

MWENYEKITI  wa  Kamati ya Kitaifa ya Maaskofu na Mashehe ya Maadili Amani na Haki za Binadamu kwa Jamii ya Madhehebu ya Dini Nchini, Askofu William Mwamalanga,  amemshauri  Rais Samia Suluhu Hassan, kuendelea kufanya marekebisho  makubwa  taasisi za  fedha ili  wananchi  wa hali chini waweze kuingia kwenye biashara  ndogo ndogo  na kubwa.

 Aidha,  Askofu Mwamalanga  amesema wananchi  wengi wanaachwa mbali kutokana  na uwezo mdogo wa kifedha  huku wengine  wakiingia kwenye  mikopo kausha damu.

Askofu Mwamalanga alitoa ushauri huo jana kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari. 

Alisema Rais Samia akifanyia taasisi za fedha mabadiliko makubwa zitawezesha wananchi kupata mikopo kwa urahisi na kuondokana na mikopo ya kausha damu.

Aidha, alimshauri Rais Samia  kuingilia kati ili Wazabuni  wanaolisha shule na vyuo  waweze kulipwa madeni yao ambayo wanadai kwa muda mrefu. “”Hawa  Wazabuni  ndiyo  wanalisha watoto chakula kwenye  vyuoni na shule za bweni lakini  wengine  hawajalipwa kwa miaka mawili  hadi leo..

 Serikali inapolipa  madeni kwenye  taasisi  na watu binafsi  kama Wazabuni  na makandarasi  kwa wakati njamii ya chini inanufaika  kwani  hao ndiyo  vibarua.

“Baadhi  ya Wazabuni  kutoka  mikoa ya  Rukwa , Katavi na Songwe wameonesha kukataa tamaa kutokana na  madhara makubwa  yanayo wakutana kwa zaidi ya  miaka mitatu  ya kukosa fedha  za malipo yao. .Alisisitiza kwamba Serikali inapochelewesha malipo  ya wazabuni  inahatarisha afya   wanafunzi  vyuoni na mashuleni