Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online DSM
ZIARA ya mbalimbali za nje ya nchi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan zimeendelea kuleta tija kwa Taifa mara baada ya Shirika la Nyumba la Taifa kupokea Wawekezaji kutoka Jamhuri ya Korea Kusini ukiongozwa na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Fedha ya Korea kwaajili ya Ujenzi (K-Finco), Dkt. Lee Eun Jae ameonesha kuguswa na NHC linavyotekeleza miradi yake kwa ubora na kwa kiwango cha Kimataifa.
Wawekezaji hao wamepokelewa leo Julai 27,2024 baada ya ujumbe huo ambao pia umeongozwa na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Jamhuri ya Korea Kusini, Mheshimiwa Togolani Mavura kuitembelea baadhi ya miradi ya shirika hilo jijini Dar es Salaam.
Ujumbe huo upo nchini kufuatia wito wa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan wa kuchangamkia fursa za uwekezaji katika sekta ya nyumba na maeneo mengine.
Awali, Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), William Genya amewaonesha wajumbe hao eneo la Upanga Mashariki jijini Dar es Salaam ambalo linatarajiwa kuendelezwa na shirika hilo kwa kushirikiana na wadau.
Vile vile ujumbe huo umetembelea mradi wa NHC, Kawe Seven Eleven (7/11) ambapo wameshuhudia utekelezaji ukifanyika kwa kasi kubwa.
Kazi waliyoikuta imefanyika ni kubwa, ambapo mradi huo kupitia majengo marefu ya kisasa yameanza kubadili mandhari ya Kawe na kulifanya eneo ulipo mradi kuwa la kuvutia zaidi.
Kilichowavutia zaidi wajumbe hao ni kushuhudia ujenzi huo ambao unatekelezwa na kampuni ya ujenzi ya Esteem Construction, wazawa wanafanya kazi kwa bidii.
7/11 huu ni mradi wa makazi ambao pia unajumuisha maduka kwa ajili ya kupangisha watu mbalimbali.
Katika nyumba za makazi zimegawanyika katika makundi mbalimbali ikiwemo ya vyumba viwili, vitatu na vinne.
Aidha, nyumba za vyumba vitatu zimegawanyika katika makundi mawili kwa maana ya vyumba vya kawaida na kundi lingine ni la ghorofa ndani ya ghorofa.
Mkurugenzi wa Ubunifu wa NHC, Emmanuel Moshi ameueleza ujumbe huo kuwa, mradi wa 7/11 ni miongoni mwa miradi ya kisasa zaidi ambayo inatekelezwa na shirika hilo.
Mradi huu ulikuwa umekwama kwa miaka kadhaa, lakini baada ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuingia madarakani aliruhusu shirika kuchukua mkopo ili kuukwamua, matokeo yake tangu mradi uanze mapema mwaka huu mambo yamekuwa mazuri zaidi na kila mtu anatamani kuwa na nyumba ndani ya mradi.
More Stories
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili
ACT-Wazalendo,waitaka Polisi kutobeba chama kimoja