Na Bakari Lulela ,Timesmajira
WAKALA wa vipimo (WMA) mkoa wa kinondoni jijini Dar es salaam, wamemkamata kijana moja mkazi wa mbezi beach Denis Chacha (22)muuza bucha kwa kosa la kutumia mzani danganyifu kwa wateja, ambao haujahakikiwa na Wakala hao.
Hayo yamebainishwa leo jijini wakati ambao Wakala wa vipimo walipokuwa wakifanya zoezi la kustukiza mahala hapo ndipo walipo baini hujuma zinazofanywa na watoa huduma wa nyama kuwa si rafiki kwa wateja wao.
“Mara kadhaa kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi dhidi ya upunjwaji wa huduma hiyo ambayo hutokana na watoa huduma hao kutumia mizani isiyo na sifa kujipatia faida ,”amesema Felix
Aidha Felix amesema kuwa wao kama Wakala wamebaini ubadilifu huo baada ya kupata malalamiko kutoka kwa baadhi ya wakazi wanaoshi maeneo hayo ya mbezi beach.
Afisa huo ameeleza namna ya kutambua mizani iliyokwisha hakikiwa na wakala wa vipimo ni pamoja na kuona mizani ikiwa na stika maalumu upande wa mbele na Ile ya kidijitali ambayo Huwa na stika pembeni.
Hata hivyo wauzaji wengi wa mabucha hutumia mizani yenye sahani mbili, moja kati ya hiyo Huwa ni yenye kupunja wateja ila nyingine Huwa ni halali kwa utoaji wa huduma hiyo.
Wakala wa vipimo kutokana na utaratibu na kanuni zao amesema hufanya kaguzi za kustukiza mara moja kwa mwaka ila wanapopata Taarifa za ukiukwaji kutoka kwa watu wema hufika mara moja kuhakiki mizani inayotoa huduma kinyume na taratibu.
Afisa wa Wakala hao amesema kuwa wafanyabiashara wanaokaidi maagizo yanayotolewa na Serikali ikiwa pamoja na kuendesha biashara bila kuhakiki mizani yao hushtakiwa kwa mujibu wa Sheria za vipimo.
Kwa upande wake mteja aliyefika mahala hapo kwa kujipatia bidhaa hiyo, Saleh Abdallah amesema wamekuwa wakipata bidhaa ya nyama kwa kupunjwa hivyo anawashukuru Wakala wa vipimo kwa kufanya kaguzi za kustukiza ambayo ni mwarubaini kwa wauzaji ambao si wema.
More Stories
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi
Mbunge Ndingo:CCM imejidhatiti kuwaletea maendeleo wananchi