September 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wadau sekta ya nafaka wakutana Dar

Na Bakari Lulela,Timesmajira

WADAU wa sekta ya nafaka kutoka nchi Tisa wamekutana jijini Dar es salaam kwa lengo la kubaini vikwazo vilivyopo katika mipaka yao na namna ya kuviepuka ili waweze kufanye biashara hizo katika mazingira salama.

Miongoni mwa nchi hizo ni pamoja na Tanzania, Zimbabwe na Afrika ya kusini.

Akizungumza jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Opla,Irene Ulola amesema lengo kubwa la kikao hicho ni kuona namna serikali zao zinawezaje kuwasaidia wadau wa bidhaa hiyo kufanya biashara kwenye mazingira mazuri ili biashara iweze kufanyike katika uwiano mzuri.

“Ili biashara iweze kufanyika katika uwiano mzuri inatakiwa kuondoa vikwazo vilivyopo katika mipaka yetu ikiwemo tozo mbalimbali ndipo waweze kukutana baina ya  muuzaji na mnunuzi,”amesema Irene 

Aidha Irene amesema kuwa vyakula vitakavyouzwa na wafanyabiashara hao vinatakiwa viwe bora na salama katika miili ya watumiaji ikiwemo wanyama na binadamu.

Ameendelea kusema mkulima  wa Nafaka akipata soko zuri ataweza kunufaika kwa kutengeneza faida yenye kukidhi hitaji lake katika masuala ya kichumi ikiwemo fedha na gharama za pembejeo.

Hata hivyo amehitaji mipakani pasiwepo na vikwazo vyovyote vitavyopelekea bidhaa hizo kuharibika ama kuoza ambapo inakuwa hasara kwa mkulima au muuzaji.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Nafaka Afrika Mashariki na Kusini Gerald Masila amesema kuwa kikao hicho kimewakutanisha wadau mbalimbali Ili kuweza kuinua hali ya wakulima wa ACG Ili waweze kufanye biashara bila ya vikwazo vyovyote.

Mkuu huyo amewasihi wadau hao kuwa pamoja katika ufanyaji wa biashara hizo kwa kuondoa vikwazo mbalimbali ambavyo havina nafasi katika sekta ya nafaka.