September 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Samia:  Tutaendelea kutekeleza Mapendekezo Tume Haki Jinai

*Akoshwa ujenzi Jengo la  Makao Makuu ya Polisi Katavi, ataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Polisi

Na George Mwigulu, Timesmajiraonline,Katavi

RAIS Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali itaendelea kutekeleza mapendekezo ya Tume ya Kuboresha Mifumo ya Haki Jinai ikiwemo kuboresha miundombinu ya Jeshi la Polisi Tanzania.

Rais Samia aliyasema hayo wakati akizindua jengo la Makao Makuu ya Jeshi la Polisi – Mkoa wa Katavi, ambapo aliwataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi hilo katika kuhakikisha ulinzi wa raia na mali zao.

Wakati akizindua ujenzi wa maghala na vihenge vya kisasa vya kuhifadhi nafaka, Rais Dkt. Samia ameielekeza Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula kuufanya Mkoa wa

Katavi kuwa kanda inayojitegemea kwenye ununuzi na uhifadhi wa nafaka.

Mradi huo ambao utasaidia kukabiliana na usalama wa chakula na kupunguza upotevu wa chakula baada ya kuvunwa, umeongeza uwezo wa Mkoa wa Katavi kuhifadhi nafaka kutoka tani 5,000 hadi tani 28,000.

Aidha, kufuatia msimu mpya wa ununuzi wa nafaka kuzinduliwa, Rais Dkt. Samia

alisisitiza umuhimu wa wanunuzi wa mazao kote nchini kuzingatia haki wakati wa ununuzi na kutoa bei nzuri kwa wakulima.

Rais Samia pia alitembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi ambao ni sehemu ya umarishaji wa huduma za afya zinazotolewa

katika Hospitali za Rufaa za Mikoa 28 chini, ikiwemo huduma za mama na mtoto.

Hali kadhalika, Rais Dkt. Samia amewahimiza wananchi mkoani humo kushirikiana na Serikali kudhibiti mimba za utotoni na kuhakikisha watoto wa kike wanapata fursa ya kusoma.