Na Penina Malundo,Timesmajira
KAMPUNI ya Ujenzi wa Miundombinu,Usafirishaji na Usambazaji wa Umeme nchini (ETDCO)imetoa wito kwa wananchi,Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)na Wakala wa Usambazaji Umeme nchini (REA)kuendelea kujitokeza kwa wingi na kufanya kazi nao ili kuweza kukamilisha ujenzi wa miundombinu kukamilika kwa wakati.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi wa Huduma za Ufudi kutoka Kampuni ya ETDCO,Mhandisi Dismass Massawe wakati wa maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara ”Sabasaba”,amesema Kampuni yao ni kampuni Tanzu iliyopo chini ya Shirika la Umeme ambayo ilianzishwa mwaka 2016 na kufanya shughuli mbalimbali za ujenzi wa miundombinu ya umeme.
Amesema lengo kuu ya kampuni hiyo kuanzishwa kwaajili ya kufanya kazi zote za ukarabati na ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji na usambazaji umeme nchini ambapo kwa sasa kampuni hiyo inaendelea na majukumu katika maeneo mbalimbali.
Mhandisi Massawe amesema wanafanya kazi hiyo mikoa yote nchini ambapo miradi ya Tanesco ipo au miradi ya REA ipo.
“Tunafanya kazi kwa msogo wote level yote na tunaanza ujenzi wa umeme wa usafirishaji Kilovoti 220,mbali na hilo pia tunamradi ya usafirishaji umeme wa Kilovot1 132 na Kilovoti 33 na mwingine Kilovoti 11,”amesema na kuongeza
”Tunafanya kazi ya kuunganisha wateja katika miradi mbalimbali ambayo tumefanya Tanzania nzima hii miradi tunapata kupitia REA ambapo kwa sasa tunamiradi mingi ikiwemo mkoani Katavi,Geita,Kigoma,Tabora,Dar es Salaam (hii ya kukarabati umeme) na mkoani Mbeya.”amesisitiza
Aidha amesema kwa sasa wanatekeleza miradi ya msongo wa kilovote 220,132 na 33 na ujenzi wa vituo vya kupooza umeme wa msongo wa kilovote 22 kwenda 33.
Mhandisi Massawe amesema pia wanamiradi katika mikoa 10 kwa sasa ambayo ni Mkoa Mbeya,Mtwara,Lindi,Dododoma ,Katavi,Pwani,Dar es Salaam ,Geita,Kigoma na Arusha.
‘Natoa wito kwa Wananchi wajitokeze kuja kutuona kwa wale wanaotaka kufanya kazi na sisi tunawakaribisha watu binafsi,Tanesco na Rea katika kufanya kazi,sisi tunafanya kazi kwa kufata ubora wa hali ya juu kwani tumeaminiwa chini ya Tanesco kwaajili ya Ujenzi na Ukarabati wa miundombinu ya umeme nchini,”amesema.
More Stories
Walimu elimu ya lazima watatakiwa kuwa wabobezi kwenye masomo wanayofundisha
Wahakikishiwa usalama siku ya kupiga kura
CCM inabebwa na kazi nzuri za Rais Dkt. Samia-Makalla