January 24, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

JMAT watembelea banda la Kampuni ya Superdoll Tanzania

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

UONGOZI wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) ikiongozwa na mwenyekiti wake Taifa Shekh Alhad Mussa Salum wametembelea banda la Kampuni ya Superdoll Tanzania kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara kimataifa Dar es salaam SABABASA, kujionea bidhaa mbalimbali ambazo zinazalishwa na kusambazwa na kampuni hiyo.

Akizungumza na katika Maonesho hayo jana Julai 2, 2024, ,Meneja wa Maendeleo ya Biashara Superdoll Bw.Adam Lubago amewakaribishwa wananchi wote kutembelea banda lao kujifunza na kujionea bidhaa mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo.

Amesema bidhaa za kampuni hiyo ni imara na zinadumu kwa muda mrefu ambapo miongoni mwa bidhaa hizoo ni pamoja na bidhaa za kisasa za kubeba mizigo ambazo hazitoi hewa ukaa na vilevile kampuni hiyo inatambulika kwa kuzalisha trela madhubuti zinazodumu kwa muda mrefu.

“Mpaka leo hii unaweza kukutana na trela ambazo tulizitengeneza zaidi ya miaka 25 bado ziko barabarani, utakuta zimeandikwa doll au superdoll”amesema.

Aidha Bw.Lubago ameeleza kuwa wanauza spea za magari,vifaa vya gereji,vifaa vya kubeba mizigo mikubwa, sambamba na Jenereta kubwa zisizotoa sauti ambapo zinajiendesha kiotomatiki.

Pamoja na hayo Lubago amesema wanatoa huduma ya mataili mbalimbali kutoka kampuni tofauti tofauti ambapo amebainisha kuwa yapo kwa ajili ya magari ya migodini,magari madogo pamoja na makubwa.