Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online DSM
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii yaipa kongole Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa kusimamia vyema miradi ya Samia Housing Scheme,Kawe 711 na Morocco Square ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kwa viwango inavyostahili kutokana na kazi nzuri aliyoifanya ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwaajili ya kuendeleza miradi iliyokuwa imesimama inayotekelezwa na Shirika hilo.
Akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kukagua miradi hiyo mitatu inayotekelezwa na Shirika hilo leo Juni 30,2024 Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii Timotheo Mzava, amebainisha kuwa uamuzi wa Rais Dkt. Samia kutoa kibali kwa NHC kuendelea na utekelezaji wa miradi yake ni wakizalendo na kwamba NHC kwa sasa hawana kisingizo cha kutokamilisha miradi hiyo kwa wakati.
Mzava amesema, baada ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuona tatizo hilo alitoa kibali ili shirikalipate fedha liweze kuikwamua miradi hiyo na matokeo mazuri yameonekana, kwani miradi hiyo ipo katika hatua nzuri.
Naye, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Geophrey Pinda amesema kuwa miradi ya Samia Housing Scheme,Kawe 711 na Morocco Square ipo katika hatua nzuri na kwamba mradi wa Morocco Square umeshakamilika kwa asilimia 99 na tayari majengo yaliyopo yameshachukuliwa na wapangaji na wanunuzi kwa asilimia 90, hiyo ni ishara kuwa miradi hiyo sasa inafanya vizuri kutokana na uamuzi mkubwa uliyofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutoa kibali ili kutekelezwa kwa Miradi hiyo.
“Tunamshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuridhia miradi hii kuendelea, na kwa sasa, jengo la Morocco Square limekamilika ambalo lilikuwa linakaliwa na watu watatu, baada ya uwekezaji huo wa NHC, eneo hilo sasa litakuwa na makazi mengi ikiwemo vitega uchumi vya kutosha.
Pia, amesema wataendelea kusimamia maelekezo ya Rais Dkt. Samia ili kuhakikisha miradi hiyo inamalizika kwa wakati na kuhakikisha inaleta tija kwa wananchi ,shirika na Taifa kwa ujumla.
Aidha, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Hamad Abdallah amsema kuwa hadi sasa katika nyumba za makazi na biashara zilizouzwa na Shirika limekusanya kiasi cha Bilioni 30 na kiasi cha bilioni 35.9 kinaendelea kukusanywa huku eneo la maduka limeshapangishwa kwa asilimia 98 ambapo kwa sasa upangaji wa bidhaa unaendelea ili kufungua maduka hayo mwezi Julai mwaka huu.
“Eneo la maduka (mall) limeshapangishwa kwa asilimia98 na kwa sasa upangaji wa bidhaa unaendelea ilikufungua maduka hayo mwezi Julai, 2024, kwa upande wa mradi wa 7/11 amesema, mradi huo wenye nyumba 422 pamoja sehemu yabiashara wa Kawe 7/11 ulianza Novemba 2014 naulisimama 2018”.
Amesema,mkandarasi alirejea kuendelea na ujenziJanuari, 2024 ambaye ni Estim Construction CompanyLimited kwa gharama ya shilingi bilioni 169.9 na kwasasa ujenzi umefikia asilimia 40, Mradi unatarajiwa kukamilika mwezi Aprili, 2026.Mauzo ya nyumba katika mradi huu yanaendeleaambapo shirika limekusanya shilingi bilioni 2.9 nalitazindua rasmi mauzo ya mradi huu Julai, 2024.”
Hata hivyo, amewataka Watanzania kuchangamkia fursaza manunuzi ya nyumba hizo kwani, anayefanya malipomapema ndiye anapata nafuu kubwa kulikoanayesubiria mradi ukamilike.
More Stories
Mhandisi Samamba awasisitiza maafisa madini kusimamia usalama wa migoni msimu wa mvua
Wapinzani kutimkia CCM ishara ya ushindi Uchaguzi Serikali za Mitaa
Vikundi Ileje vyakabidhiwa mikopo ya asilimia 10, DC Mgomi avipa somo