Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imekutana na wateja wake wakubwa yaani makamppuni na taasisi mbali mbali (Corporates) wa jijini Arusha ili kujadili fursa za biashara, kutambulisha huduma mpya za benki hiyo sambamba na kuwaejengea uelewa zaidi wateja hao kuhusu faida na manufaa ya huduma hizo.
Benki hiyo pia ilitumia fursa hiyo kujadili na wateja hao namna inavyoweza kuboresha huduma zake kulingana na mahitaji yao.
Akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki hiyo kupitia timu yake ya Biashara na Uwekezaji (CIB) mwisho wa wiki hii jijini Arusha, Mkurugenzi wa wateja wakubwa, taasisi binafsi na za serikali kutoka NBC , Bw James Meitaron alisema tukio hilo ni muendelezo wa matukio kama hayo mahususi kwa wateja wakubwa katika mikoa mbalimbali hapa nchini ikiwemo Dodoma, Mwanza na Arusha.
“Tukiwa kama muhimuli muhimu wa utoaji wa huduma za kifedha nchini, NBC tunatambua umuhimu wa utoaji wa huduma bora kwa wateja na kukuza ushirikiano kati yetu na wateja wetu. Hii inasababishwa na mabadiliko yanayotokana na ubunifu na maendeleo ya kiteknolojia.’’
”Hivyo hatua hii ya kukutana na wateja wetu wakubwa inatoa fursa kwetu kuelezea maboresho makubwa tuliyofanya kwenye huduma zetu sambamba na kutambulisha huduma mpya zilizorahisishwa zaidi kidigitali na zinazoendana na mahitaji ya wateja wetu hususani hawa wakubwa.’’ Alisema
Aidha, kupitia mpango huo benki hiyo imekuwa ikielezea mikakati yake mipana inayolenga kuwahudumia kwa ufanisi zaidi wateja hao, kuwajengea mitandao ya kibiashara miongoni mwao sambamba na kuwasogezea huduma za kibenki karibu zaidi huku huduma ya NBC Connect ikitajwa kama suluhisho muhimu katika kuwasogezea huduma za kibenki wateja hao wakubwa yakiwemo mashirika na kampuni binafsi, pamoja na taasisi za serikali.
“Tunaamini kuwa msingi wa huduma za kipekee ni kuelewa mahitaji na matakwa ya wateja wetu, ziara hizi zinatupatia mitazamo au maono yatakayosaidia kuwa wabunifu na kuboresha uzoefu wa kibenki kwa ujumla.” Aliongeza Bw Meitaron.
Bw Meitaron alitaja baadhi ya mambo muhimu ambayo benki hiyo imekuwa ikiyanzingatia katika kukuza ushirikiano na taasisi za kibiashara hapa nchini kuwa ni pamoja na utoaji wa suluhisho zenye ubunifu katika huduma za kifedha, Ubunifu wa kiteknolojia, Ubia wa kimkakati, Kukuza Ukuaji wa Uchumi pamoja na Uwajibikaji kwa jamii huku kipaumbeke kikiwekwa zaidi kwenye masula ya Elimu, Afya na uhifadhi wa mazingira.
“ Hivyo basi NBC tunazialika jumuiya za wafanyabiashara kuangalia fursa na faida za kushirikiana na taasisi ya fedha ambayo ina dhamira ya dhati na mafanikio yao, kwa kukuza ushirikiano na kutoa zana zinazohitajika katika ukuaji. NBC inalenga kuwa mshirika mwaminifu anaayetegemewa katika biashara hapa nchini,’’ alibainisha.
Wakizungumzia hatua hiyo baadhi ya wateja wa benki hiyo mkoani Arusha walisema imekuja wakati muafaka hasa katika kipindi hiki ambacho mkoa huo upo kwenye mapinduzi makubwa ya kiuchumi kutokana ustawi mkubwa wa sekta ya utalii ikiwa ni matunda ya jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan kupitia mkakati wake wa Royal Tour.
“Kwa sasa mkoa wa Arusha tupo kwenye kasi kubwa ya mabadiliko ya kiuchumi yanayochagizwa na ukuaji wa sekta ya utalii, biashara, kilimo na viwanda. Ni habari njema kwetu kuona kwamba benki ya NBC ambayo inahudumia wadau wengi kwenye sekta hizi pamoja na wafanyakazi wa serikali wanatuunga mkono kupitia huduma zao za kisasa ikiwemo zile za kidigitali ambazo kiukweli zimekuwa msaada mkubwa hususani kwenye huduma za miamala ya kifedha na makusanyo ya serikali,’’ alisema mmoja wa wateja.
More Stories
Rais Samia amlilia Dkt. Ndugulile
Makada wa CHADEMA,mbaroni kwa tuhuma za kukimbia na karatasi za kura
Rais Samia afanya uteuzi wa viongozi mbalimbali