Na Bakari Lulela, TimesMajira Online
WAZAZI wametakiwa kuwajengea misingi imara watoto wao Ili wawe jamii yenye maadili katika kulitumikia Taifa lao katika siku za mbeleni.
Hayo yameelezwa jijini Dar es salaam na katibu wa shirika la wanaume wanaopitia changamoto za kwenye ndoa (SHIWACHANDO) katika maadhimisho ya siku mtoto wa Afrika yaliyofanyika katika ukumbi wa karimjee.
“Wazazi wakiume tuwaje watoto wetu katika misingi Bora Ili baadae wawe wenye kutegemewa hivyo tusiwaachie akina mama peke yao,” amesema Shija
Aidha Shija ameeleza kuwa malezi ya watoto pia wasiachiwe madada wa kazi kwa kuwa wao si wenye kuwapatia malezi sahihi yenye kutimiza ndogo zao za baadaeni.
Hata hivyo wengi wa akina baba wanashindwa kutimiza majukumu yao kwa kuzikimbia familia zao kwa kuzaa watoto wenye ulemavu ambapo mwenyezimungu ndiye aliyewajaalia.
Amesema nawaasa wanaume wenzangu waache mifumo dume ambao ni hatarishi kwa familia na ndoa za mitaala pamoja na ulevi wa kupindukia Ili waweze kuzitunza familia zao.
Kwa upande wake mjumbe wa shirika Hilo Michael Lugendo amesema watoto ni hazina kwa siku za usoni hivyo tuitunze vema Ili waweze tufaa katika maisha ya Dunia na ahera .
Mjumbe huyo ameitaka serikali iweze kuliwezesha kundi la wanaume Ili liweze kubuni mikakati mbalimbali ya kujiimarisha kisekta za uzalishaji, biashara na maendeleo zaidi.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba