Na Mwandishi wetu,Timesmajira
BENKI ya Biashara Tanzania (TCB), imetagaza faida ya shilingi billioni 19.27 katika kipindi cha miezi mitano tangu kuanza kwa mwaka huu .
Akitagaza faida hiyo Jijini Dar es salaam na mapema Juni 18, 2023 Mkurugenzi Mtendaji wa TCB, Adam Mihayo, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano Mkuu 32 wa wanahisa.Amesema katika kipindi hicho benki hiyo imeshuhudia ongezeko hilo la mapato ya jumla kwa shilingi Billioni 19.27 sawa na asilimia 11.19 hadi kufikia Shilingi Billioni 192.1 ikilinganishwa na mwaka 2022 ambapo mapato yalikuwa Shilingi Billioni 172.83 sawa na asilimia 1.72.
” Tunaishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutuongezea mtaji ambao umetuwezesha kufikia mafanikio haya pia …kupitia mipango ya TCB ya kimkakati na ubunifu, tumeweza kudhihirisha mafanikio makubwa ya kifedha na ya kiutendaji.”amesema Mihayo
Vilevile amesema ndani ya mwaka 2023, mali za TCB Benki ziliongezeka kutoka Shilingi Trilioni 1.285 mwishoni mwa mwaka 2022 hadi Sh. Trilioni 1.389 mwishoni mwa mwaka 2023 sawa na ongezeko la asilimia 8.1 sawa na Sh. Bil. 103.9.
“Ongezeko la mali lilichagiwa na ongezeko la amana za wateja ambazo ziljongezeka kwa asilimia 12.01 kutoka Shilingi trilioni 1 mwishoni mwa mwaka 2022 hadi kufikia trilioni 1.12 mwishoni mwa mwaka 2023″amesema Mihayo
Kwa upande wa mikopo amesema iliongezeka kwa Shilingi Billioni 73.1 kutoka Shilingi Billioni 839 mwishoni mwa mwaka 2022 na kufika Shilingi Billioni 911.2 Desemba 31, 2023 na kuonesha ongezeko la asilimia 12.01 kutoka trilioni mmoja mwishoni mwa mwaka 2022 na kufikia trilioni 1.12 mwishoni mwa mwaka 2023.
Vilevile amesema kupitia usimamizi wa kimkakati wa uwekezaji Amana za TCB Benki katika Benki nyingine zilishuka kwa shilingi billioni 55.3 huku Amana za Serikali zikiongezeka kwa shilingi billioni 44.1 na fedha taslimu na Salio katika Benki kuu ya Tanzania BoT iliongezeka kwa shilingi Billioni 47 au 41.26.
“Sisi kama benki, dhamira yetu ya kudumisha ufanisi na kumridhisha mteja inatupa hamasa na uthubutu wa kujituma zaidi ,”alisema Mihayo.Pia amesema wamedhamiria kusikiliza na kuelewa mahitaji ya wateja huku wakihakikisha wanawawezesha kupata la kifedha katika mahitaji YaoKwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi, Martin Kilimba amesema kwa mwaka ujao wa fedha, tunakusudia kuendelea kuboresha ufanisi wetu ili kuwezesha ukuaji wa taasisi hii.
“Malengo yetu ni kuendelea kuboresha mizania, kujenga taswira mpya ya taasisi yetu, kupokea teknolojia ya kidigitali, kufanya uhakiki wa hasara na kusimamia rasilimali watu.amesema Kilimba
Naye Mwenyekiti wa bodi Dkt Edmund Mndolwa aliyemaliza mda wake alitoa shukrani kwa Rais Dkt Samia Suluhu na Kwa Hayati John Magufuli kwa kumchagua na kumteua kuendesha Benki .
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba