November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wananchi watakiwa kutowahifadhi wahamiaji haramu

Na Raphael Okello, Mwanza,

IDARA ya uhamiaji mkoani Mwanza imewataka wananchi kutokomeza uhamiaji haramu kwa kutowaingiza nchini na kuwahifadhi wahamiaji haramu kwa kuwa wanaweza kuleta madhara makubwa nchini.

Hayo yamesemwa leo Jijini Mwanza na Kamishina Msaidizi Mwandamizi, Afisa Uhamiaji Mkoani Mwanza Colla Kayumba alipokuwa akizungumza wakati wa.kampeni ya “umjue jirani yako” inayoendelea mkoani Mwanza.

“Wahamiaji haramu wanayo madhara makubwa kwa usalama wa taifa letu hivyo wananchi wote wakifahamiana na kuwa tayari kutoa taarifa dhidi ya wanao washuku kuwa si raia tutakomesha tabia hiyo” amesema Kayumba.

Alifafanua kuwa wahamiaji haramu wamekuwa wakiletwa hapa nchini kwa ajili ya kutumikishwa katika shughuli za majumbani, viwandani na kwenye mashamba.

Amesema wahamiaji Harambe wengi wao ni mataifa ya Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda,Somalia, Ethiopia,Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na baadhi ya mataifa ya bara la Asia ambao huingia na kukaa bila kibali.

Amesema kampeni hiyo inahusiana na utoaji wa elimu kupitia redio za kijamii, taasisi za umma na binafsi, mikutano ya hadhara, vikao vya ndani ambapo maafisa uhamiaji na watumishi wa idara hiyo wanahusika kutoa elimu hiyo kwa jamii.

Kayumba amesema elimu ya uraia ndo suluhisho la kudumu dhidi ya matukio ya wahamiaji haramu .

Amebainisha kuwa wahamiaji haramu huletwa na watu ambao ni wenyeji wa sehemu husika hivyo kutokana na elimu ya “Mjue Jirani yako ” inayotolewa
wahamiaji haramu nchini.