October 8, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwenezi Chuji: Mnyamani hawataki viongozi wanafki

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

MWENEZI wa Chama cha Mapinduzi CCM kata ya Mnyamani Lauriani Samweli Ndunabo , amesema Kata ya Mnyamani awataki viongozi wanafiki badala yake wanataka viongozi wachapa kazi kwa ajii ya kukitukimikia chama cha Mapinduzi CCM.

Mwenezi Laurian Samweli (Chuji)alisema hayo wakati wa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Maruzuku Rashid Akungwa alipokuwa akiwashirisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya chama akiekezea yale akiyofanya katika uongozi wake.

“Kata ya Mnyamani ccm atutaki viongozi wanafiki tunaomba mfanye kazi na wakati wa uchaguzi ukifika yule Mwenyekiti atakayepita wote tumuunge mkono katika kupeperusha bendera ya chama ccm iweze kushika Dola ipange Serikali yake “alisema Lauren Chuji

Mwenyekiti wa ccm wilaya ya Ilala Said Sidde alipongeza uongozi wa kata ya Mnyamani kwa kufanya siasa safi ndani ya kata hiyo kwa kushirikiana na Serikali sasa hivi Mnyamani maendeleo makubwa kwa kuwa na miradi mikubwa ya Serikali ikiwemo sekta ya Elimu msingi na sekta ya afya .

Aidha Mwenyekiti wa ccm wilaya Sidde alimpongeza Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Maruzuku Rashid Akungwa, kwa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya chama na kuelezea Mapato na matumizi kwa kipindi cha uongozi wake na mambo aliyotekeleza ambapo amewatendea haki wananchi wake wa mtaa wa Maruzuku.

Mwenyekiti Sidde alisema Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Maruzuku Rashid anatosha kuendelea Serikali za mitaa hivyo chama kimshawishi kuchukua fomu na kuwataka wananchi wa Mnyamani mtaa wa Maruzuku kuangalia mazuri aliyofanya Mwenyekiti wao hivyo waendelee kumchagua kushika dola .

Aidha aliwataka Wana CCM Mnyamani kuchagua viongozi wanao jiuza ndani ya chama na nje ya chama ili aweze kupeperusha Bendera ya CCM.

Mwenyekiti wa CCM Mnyamani Mbaraka Mwinyimkuu aliwapongeza Mnyamani kwa kufanya usajili wa kadi za kisasa za electonic ambapo kwa sasa chama hicho kimejipanga kwa ajili ya kushika dola kata ya Mnyamani Serikali ya Dkt samia suluhu Hassan imefanya mambo makubwa kwa kutekeleza Ilani ya chama kwa kushirikiana na Mbunge wa Segerea Bonnah Ladslaus Kamoli na Diwani wa Kata ya Mnyamani Shukuru Dege.

Diwani wa Kata ya Mnyamani Shukuru Dege alisema katika mtaa wa Maruzuku Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo Rashid Akungwa alikuwa akishirikiana katika mambo ya maendeleo hivyo anatosha kuendelea kama uchaguzi leo ameshapita bila kupingwa.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Maruzuku Rashid Akungwa alisema katika uongozi wake baadhi ya mambo aliyotekeleza ikiwemo kuboresha miundombinu kujenga Barabara,Kusomesha wanafunzi ,kujenga madaraja hayo yote amefanya kwa kipindi cha miaka mitano ya uongozi wake kwa mapenzi yake ya kupenda chama.