October 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mahakama yatambia mageuzi ya Samia

*Yasema ameongeza bajeti kutoka bil. 155/- hadi bil 241.6/- mwaka 2024/2025 mifumo ya TEHAMA yarahisisha utendaji kazi, mashauri

Na Joyce Kasiki,Timesmajiraonline, Dodoma

MTENDAJI Mkuu wa Mahakama, Elisante Ole Gabriel, ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuongeza bajeti ya mahakama kutoka sh. bilioni 155 mwaka huu wa fedha unaoishia Juni 30 hadi kufika sh. bilioni 241.6 kwa mwaka 2024/2025.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dodoma, kuhusu miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt. Samia kwa taasisi hiyo ya Mahakama Prof.Ole Gabriel alisema hatua hiyo inaonesha ni jinsi gani Serikali inathamini na kutambua majukumu yanayofanywa na taasisi hiyo .

Kufuati hali hiyo, amesema kumekuwa na maboresho makubwa katika taasisi hiyo ikiwemo matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na Habari (TEHAMA).

Amesema matumizi ya teknolojia hiyo yamerahisisha utendaji kazi wa Mahakama na kuondoa usumbufu kwa wananchi kuhudhuria mahakamani.

“Hivi sasa tunayo mifumo ambayo inarahisisha utendaji kazi wa mahakama, kwa mfano tunao mfumo wa Ofisi Mtandao, ambapo mashauri mengi yanaendeshwa kwa njia ya mtandao

“Ofisi mtandao tayari inafanyika ndani ya mahakama na inawezesha watu kufanya kazi bila kuwa ndani ya ofisi zao, hata wakiwa nje au ndani ya nchi kazi zinaendelea kufanyika,”amesema.

“Na Mfumo huu unatembelewa na wadau kwa zaidi ya asilimia 82.4 na nchi inayotufuatia inatembelewa na wadau kwa asilimia 2.7,” amesisitiza.

Vile vile alisema upo mfumo wa TTS ambao husaidia kufanya ukalimani wa hukumu zote unafanya udukuzi wenyewe na unaweza kuandika lugha ya kingereza au kiswahili.

Aidha, amesema Mahakama imeanzisha kituo cha kupiga simu kwa ajili ya kupata mrejesho wa taarifa kwa namna gani wananchi wanaridhika na utendaji wa mahakama na kurudisha mrejesho ili kuzifanyia kazi changamoto zilizobainishwa na wananchi.

Kwa mujibu wa Prof. Elisante kutokana na mifumo iliyopo katika mahakama, wananchi wanaweza kufungua kesi kupitia tarehe ya kesi yake na hata kupata nakala ya hukumu kwa njia ya mtandao.

Hata hivyo amesema licha ya kazi kurahisishwa na mifumo lakini bado kuna changamoto ya wanabchi kutaka kufika mahakamani kwa jambo ambalo lingeweza kufanyika kupitia mtandao.

Aidha alisema taasisi hiyo inaemswlea kuelimisha umma kupitia wasanii na vyombo vya habari kuhusu matumizi ya mifumo hiyo ili waweze kuitumia.