Na Moses Ng’wat,Timesmajiraonline,Mbozi.
JESHI la polisi Mkoa wa Songwe limeeleza kupata mafanikio mahakamani kwa watuhumiwa wa makosa mbalimbali kuhukumiwa, ambapo watuhumiwa mbalimbali wamepatikana na hatia ya kufungwa gerezani, akiwemo Yusufu Simbeye (28) aliyefungwa jela miaka 10 kwa kosa la kufanya mapenzi na mwanamke mwenye changamoto ya afya ya akili.
Hayo yamebainishwa leo, Juni 5,2024 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Agostino Senga, wakati akizungumza na waandishi wa habari kwa lengo la kutoa taarifa ya utekelezaji wa jeshi hilo katika kipindi cha mwezi Mei, 2024.
Kamanda Senga amesema, Simbeye alipatikana na hatia hiyo na kuhumiwa kifungo cha miaka 10 jela kupitia kesi ya jinai namba 11722 iliyoendeshwa na Mahakama ya Wilaya ya Mbozi.
Kamanda Senga alitaja mafanikio mengine ambayo jeshi hilo limeyapata mahakamani katika kipindi cha mwezi Mei, 2024 kuwa ni kufugwa miaka 30 jela kila mmoja kwa watuhumiwa wengine watatu katika wilaya ya Momba.
Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni, David Simwanza (32) aliyehukumiwa kwa kosa la kufanya mapenzi na ndugu yake wa damu (maharimu)katika kesi namba 202/2024, pamoja na Ngasa Maige(25) na Simon Mwakasula (30) wate wakazi wa Wilaya Momba waliokuwa wakitumiwa na kesi za ubakaji.
Alitaja mafanikio mengine ni Yohana Mwashala (36) mkazi wa Mbozi aliyefikishwa mahakamani kwa kosa la la kubaka na kumpa mimba mwanafunzi katika kesi namba 04627/2024 na kuhukumiwa miaka 30 kwa kosa la kwanza la kubaka na miaka 20 jela kwa kosa la pili kumpa mimba mwanafunzi na kesi hiyo ilihukumiwa mahakama ya Mbozi.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba