Na Mwandishi wetu, Timesmajira
KAMPUNI ya Mbeya Cement (MCCL)imetangaza gawio la shilingi 4,259 kwa kila hisa ambayo ni marejesho yaliyosubiriwa kwa muda mrefu, yakionyesha utendaji mzuri wa kampuni uliorekodiwa mwaka 2023.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa mwishoni mwa wiki kwa vyombo vya habari,inasema malipo hayo yanaashiria mabadiliko kutoka kwa gawio la mwisho lililotolewa mwaka 2014,hali inayoonyesha mafanikio makubwa chini ya umiliki mpya.
Kampuni hiyo inayofahamika kwa umaarufu wa chapa ya Tembo Cement, hivi karibuni imekuwa mwanachama wa Amsons Group, ambayo ilinunua asilimia 65 ya hisa kutoka kwa kundi la Holcim lenye makao yake Uswisi.
Ununuzi huo unatajwa kuchangiwa na uongozi mpya ulioleta Ubunifu na mikakati ya kuongeza pato la kifedha kwa kiasi kikubwa.
Taarifa zinaeleza kuwa Mafanikio hayo pia yanatokana na kupungua kwa utegemezi wa klinka iliyopatikana, kwani kampuni imeongeza uzalishaji kutoka kwenye migodi yake.
“Kwa mali zote zenye thamani ya shilingi bilioni 175.2 na madeni ya shilingi bilioni 123.8, mtaji wa MCCL ni thabiti kwa shilingi bilioni 51,” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo.
Aidha, taarifa hiyo inasema Serikali inayomiliki asilimia 25 kupitia Msajili wa Hazina, inatarajiwa kupokea takriban shilingi bilioni 3 za gawio.
Kulingana na waraka huo, Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), mmiliki wa asilimia 10, ulitarajiwa kupata shilingi bilioni 1.2 za gawio.
“Gawio hili kubwa linakuja kama msukumo wa kukaribishwa, likionyesha ufanisi mzuri wa kifedha wa kampuni na uwezo wa baadaye,” inasomeka sehemu nyingine ya taarifa hiyo.
Hifadhi kubwa za migodi ya kampuni na uwezo wa kuongeza uzalishaji wa klinka vilikuwa vipengele muhimu, “pamoja na mkutano ukisisitiza haja ya uwekezaji wa kimkakati ili kuongeza matumizi ya rasilimali hizi.
“Uplift ya kifedha ya hivi karibuni ilisaidiwa zaidi na makubaliano muhimu yaliyofikiwa Novemba 2023, ambayo yalibadilisha mkopo uliopo kutoka Cemasco Limited, kupunguza mzigo wa madeni ya kampuni na kuruhusu uwekezaji upya katika maeneo ya ukuaji.
“Hivi sasa inashikilia asilimia sita ya soko, MCCL iko tayari kupanuka. Usimamizi wa kampuni unazingatia kuboresha mikakati ya vifaa na masoko ili kuhifadhi wateja waliopo na kuvutia wapya,” inasomeka sehemu nyingine ya taarifa hiyo.
More Stories
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa
NLD kipo tayari kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa