Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
WAZIRI wa ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jery Silaa amepiga marufuku Wananchi wa kata ya Msongola kuuza ardhi kuanzia sasa badala yake wasubiri Serikali wanaupanga upya mji huo.
WAZIRI ARDHI Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jery Silaa alisema hayo kata ya Msongola katika mkutano wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM iliyowasilishwa na Diwani wa Kata ya Msongola AZIZI MWALILE.
“Ninaagiza kata ya Msongola inapangwa upya kuanzia sasa kutokana kuwa na eneo kubwa la ardhi hivyo wananchi marufuku kuuza ardhi eneo hili Wizara ya Ardhi inajipanga rasmi kuanza kutoa hati za ardhi kwa kila kila kiwanja cha mwananchi”alisema Jery.
Waziri Jery alisema mikakati ya urasimishaji ardhi unaanza rasmi hivyo marufuku pia kuuza kiwanja miguu 20 kwa 20 aliwataka wananchi wa jimbo la Ukonga kata ya Msongola ,yenye mitaa Kidole,,Mvuti Kitonga ,Yange Yange, Mondole,Kiboga,Mvuleni kutunza ardhi yao na maeneo ya wazi yasichezewe .
Akizungumzia uchaguzi wa Serikali za mitaa alisema Wenyeviti wa Serikali za mitaa waliofanya vizuri katika mitaa yao kwa kuwatumikia wananchi watarudi na watashinda kwa kishindo hivyo aliwataka Wenyeviti wa Serikali za mitaa kuchapa kazi kwa weledi.
Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Msongola MWITA MAHANDO aliwataka watendaji wa Serikali Walimu na Watumishi wa kata ya Msongola kusimamia miradi ya Serikali vizuri Mtendaji atakayerudisha nyuma maendeleo ya Serikali kwa kushindwa kusimamia miradi hatachukuliwa hatua.
Mwenyekiti MAHANDO alisema CCM MSONGOLA imesimama IMARA hivyo aliwataka watendaji Msongola kushirikiana na chama katika kuleta maendeleo ya Serikali ikiwemo kusimamia miradi ya sekta ya afya na sekta ya Elimu.
Diwani wa Kata ya Msongola AZIZI MWALILE alisema Changamoto kubwa ya kata ya Msongola MPAKA wa Mvuleni na TAMBANI hivyo ameomba wizara imsaidie katika kuweka sawa mipaka hiyo kabla uchaguzi wa Serikali za mitaa.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa