Na Penina Malundo, Timesmajira
VIJANA watatu wa Tanzania kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Ndaki ya Tehama ICT (CoICT,wamerejea nchini baada ya kuibuka washindi wa kwanza wa mashindano Mkubwa ya Kimataifa ya Huawei ICT nchini China.
Vijana hao ni Dickson Mram,Matimu ahimbo na James Amos ambao wanaujuzi katika uhandisi wa kompyuta ,IT na Mawasiliano ya simu ambapo walishiriki mashindano hayo yaliwashindanisha wanafunzi zaidi ya 470 kutoka nchi 49 duniani.
Akizungumza jana baada ya vijana hao kuwasili nchini, Kaimu Mkurugenzi Mkuu Tume ya Tehama ambaye pia ni Mkurugenzi wa Masuala ya Maendeleo ya Wataalam wa Tehama Tume hiyo,,Mhandisi Sadath Kalolo amesema mashindano ya Huawei ICT ni moja ya mashindano makubwa na yenye ushindani mkubwa duniani katika tasnia ya teknolojia ya habari na mawasiliano.
Amesema ushindi huo kwa vijana hao unathibitisha siyo tu uwezo wao wa kitaalum,bali pia ni uwezo wao wa kufanya kazi kwa bidii ,ushirikiano na uvumbuzi.
”Nawapongeza kwa mafanikio makubwa mliyoyapata huko China,ushindi wenu si tu ni heshima kwenu binafsi bali ni heshima ya nchi yetu,mmeonyesha uwezo wa hali ya juu,ubunifu na ujuzi wa Kiteknolojia ambao unatufanya sote tuwe na fahari.
” Mmeonesha kwamba mnaweza kushindana na kufanya vizuri katika jukwaa la kimataifa jambo ambalo linavutia na kujivunia kwa kiasi kikubwa,”amesisitiza.
Aidha amewasihi washindi hao kuendelea kufanya kazi kwa bidii,kujifunza zaidi na kuendelea kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya teknolojia ya habari na mawasilino ambayo itaweza kuwafikisha mbali katika malengo makubwa zaidi.
Amesema kitendo cha vijana hao kuwa nafasi ya kwanza kinajenga uwezo wa kujiamini sio kwao pekee yao bali kwa vijana wengine ambao wapo katika huduma ya tehama kuandaa bunifu zao.
”Sisi tutaendelea kuwalea vijana hawaili wajifunze zaidi na kuendelea kuongeza mchango wao katika ukuaji wa tehama nchini,Waziri amefurahi sana na ushindi huu na amehaidi kukutana nao,”amesema.
Mbali na pongezi hizo kwa vijana,amesema Tume yao ya TEHAMA inaprogramu mbalimbali ikiwemo programu mpya ya uanzishaji wa vituo vya kukuza bunifu za tehama ambavyo vitakuwa katika kanda nane nchini.
Amesema Vituo hivyo vitakuwa miongoni mwa sehemu sahihi za kulea vipaji vya tehama ili kukuza bunifu zao na kuingia sokon.”Kazi hii tunaifanya kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Vyuo vingine pamoja na Sekta binafsi kuhakikisha tunaibua vipaji hivi kwa pamoja ili kutatua changamoto zilizopo katika masuala ya Tehama,”amesema.
Akitaja maeneo ambayo vituo hivyo vitakuwepo ni pamoja na Dar es Salaam,Lindi,Mwanza,Arusha,Tanga,Mbeya na Zanzibar,ambapo vituo vitaanzishwa na vitakuwa mahususi kwa kulea na kukuza bunifu za tehama kwa vijana ambazo zitawapelekea kufika katika uchumi wa kidigiti .
Kwa Upande wake Professa Mshiriki kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Ndaki ya TEHAMA, Prof. Baraka Maiseli amesema kwa muda mrefu wamekuwa wakiwafundisha vijana wa chuo hicho masuala ya tehama na kuwalea.
Amesema kupitia ushindi huu,imewaonyesha nia ya kutoishia hapo bali kutafuta namna ya kuviendeleza vipaji hivyo na kuwasaidia kuingia katika programu za serikali ili kuweza kutatua changamoto mbalimbali ambazo zipo katika nchi ya Tanzania.
Akizungumzia ushindi huu,amesema hii inaonyesha Tanzania sasa inauwezo wa kutatua changamoto mbalimbali katika sekta ya tehama na pia kuna haja ya kutafuta vijana wenye uelewa wa masuala ya tehama na kuwalea katika masuala haya tehama.
James Magesa,Mmoja wa washindi waliotoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,amesema haikuwa ngumu kwao kwani walikuwa wakifanya maswali kwa kushirikiana na kuhakikisha wanamaliza yote.
”Sisi tulikuwa na aina yetu ya kumaliza maswali tuliyopewa ambapo tulikuwa tunamaliza yote kwa pamoja tofauti na wenzetu walikuwa wanafanya moja moja hiyo ndio mbinu iliyotupatia ushindi,”amesisitiza.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba