November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wito watolewa vijana wakike kujifunza masuala ya ujenzi

Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma

TAASISI ya Teknolojia ya Ujenzi(ICoT)imetoa wito kwa vijana wa kike nchini kupata elimu ya ufundi ili waweze kushiriki katika shughuli zinazohusiana na ujenzi kama vijana wa kiume.

Wito huo umetolewa jijini hapa leo,Mei 28,2024 na Mhandisi Paul Henry kutoka katika Taasisi hiyo wakati akizungumza na mtandao huu kwenye maonesho ya Taasisi zilizo chini ya sekta ya ujenzi Bungeni,ambapo amesema kumekuwa na imani ya wanawake kuogopa kujifunza mafunzo yanayohusu ujenzi kwa kuamini kuwa ni shughuli za wanaume kitu ambacho siyo kweli.

Mha.Henry amewatoa hofu vijana wakike wote nchini kuwa wasiamini kwamba shughuli hizo ni ngumu kwamba wao hawawezi kufanya kwani wanaweza kufanya wakati mwingine kuliko hata wanaume.

“Wito wangu wanawake wote wajue shughuli zote za ujenzi wao wananafasi kubwa yakushiriki kama wanavyoshiriki mwanaume mwingine yoyote na wasiamini kwamba hizi shughuli ni ngumu kwamba wao hawawezi kufanya,wanaweza kufanya vizuri tu
Ushuhuda ni wale ambao tayari tunawafundisha wanafanya vizuri,”amesema.

Aidha amesema kuwa katika Taasisi hiyo kuna kozi maalum ya stahiki ya nguvu kazi umeunda kozi maalumu zinaitwa kozi maalumu za wanawake ,vikundi vya wanawake na vijana na wenye uhitaji maalumu.

“Hizo kozi ukiangalia washiriki wakubwa ni wanawake kwahiyo wanavyokuja hapo tunavyowafundisha wanafanya vizuri sana kwahiyo wanawake wasifikirie kuwa hzi ni za wanaume au kwamba wao hawawezi hapana nawasihi waweze kuja na hayo mawazo yao yatatoka.

Vilevile amesema kuwa Taasisi hiyo inauwezo wa kufundisha na watu wenye mahitaji maalumu na kwani mwaka 2019 hadi 2020 walikuwa na watu wenye ulemavu wakijifunza fani za ufundi.

Hivyo ametoa wito kwa watu wenye ulemavu kutosita kwenda kupata mafunzo ya ufundi katika taasisi hiyo
huku akifafanua kwamba kwasasa hawajapata mtaalamu wa kufundisha wenye ulemavu wa macho lakini wataangalia namna ya kutafuta mtaalamu ili na wenye ulemavu wa macho wapate elimu.

Wenye Ulemavu kwa sasa hatuna ila tuliwa kuwa nayo miaka ya 2019 hadi 2020 tuliwahi kufundisha watu wenye ulemavu ila kwasasa hatuna hatujapata uwezo wa kuwafundisha tunao ila kwa ulemavu wa macho bado hatujapata mtaalamu wa kuwafundisha.

Pamoja na hayo Mha.Henry ameeleza kuwa Taasisi hiyo ipi chini ya Wizara ya ujenzi imeanzishwa na kusajiliwa na Baraza la Elimu ya ufundi stadi(NACTVET) mwaka 2021 ambapo inatoa mafunzo ya ufundi kwa ngazi ya National Technical Award(NTA)daraja la 4 hadi 6 na mafunzo ya ufundi stadi ngazi ya Vacational Education Training (VET) daraja la 1 hadi 3.