Na Jackline Martin, TimesMajira Online
RAIS Samia Suluhu Hassan anatarajiwa
kuwa mgeni rasmi katika Mkutano wa Uvuvi Barani Afrika wenye lengo la kuimarisha umoja wa Afrika na kuwasilisha maoni ya Mkutano huo katika mikutano ya kimataifa kama Sauti Moja ya Afrika.
Hayo yamesemwa jana na Waziri wa
Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega wakati
akizungumza na waandishi wa habari Jijini
Dar es Salaam kuhusu ujio wa mkutano
huo.
Mkutano huo utafanyika Tarehe 5-7 Julai
mwaka huu katika ukumbi wa mikutano
Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
“ Pamoja na mambo mengine,
mkutano huu utatumika kama Jukwaa
litakolokutanisha wavuvi kutoka nchini
Tanzania na wenzao kujadili mafanikio
na changamoto zinazowakabili dhidi ya
mustakabali wao.”
Waziri Ulega amesema mkutano huo
utajumuisha maadhimisho ya miaka 10 ya
utekelezaji wa Mwongozo wa Uvuvi Mdogo
na Muundo wa kisera wa kusimamia uvuvi
na ukuzaji vviumbe maji barani Afrika, lakini pia utaangazia fursa zilizopo katika Uchumi wa Buluu.
“Mkutano huu utakuwa chachu ya
kubadilishana mawazo, fursa na teknolojia
mbalimbali za kuhakikisha nchi inapiga
hatua kubwa kwenye utekelezaji wa dhana
ya kujenga kesho iliyo bora kwa vijana
wetu (BBT), na kufikia malengo makubwa
kwenye Uchumi wa Buluu.”
Aidha Waziri Ulega amesema mkutano huo
unatarajia kujumuisha viongozi na wataalam wa sekta ya Uvuvi kutoka Afrika, wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa barani Afrika na Ulimwenguni kwa ujumla, Taasisi zisizo za Kiserikali, Taasisi za Kikanda, Watafiti, Vyuo Vikuu, na Wavuvi Wadogo ambao ndiyo wahusika wakuu wa Mkutano huu.
Waziri Ulega ameyataja manufaa mbalimbali ambayo nchi itayapata kupitia Mkutano huu ikiwa ni pamoja na Kufungua fursa za uwekezaji kwenye sekta ya Uvuvi, Kufungua wigo wa masoko ya nje ya mazao ya Uvuvi ya nchini Tanzania, kuongeza uwanda mpana wa wavuvi nchini kujifunza namna ya kuendesha shughuli zao kisasa ili uvuvi wao uwe na tija, kuendelea kuboresha mahusiano ya matumizi ya rasilimali za maji ya asili na zile za ukuzaji viumbe maji, baina
ya wadau wa Sekta ya Uvuvi waliopo hapa
nchini na wale wa mataifa mengine barani
Afrika na Ulimwenguni kwa ujumla.
Pia Waziri ulega ameongeza kuwa “Mkutano huo pia utachangia katika kuongeza kipato cha Mtanzania mmoja mmoja na Uchumi wa Taifa letu kwa ujumla wake.”
Mbali na hayo, Waziri Ulega almewakaribisha
wadau wote wa Sekta ya uvuvi waliopo
nchini kushiriki katika mkutano huo na
kuhakikisha wanatumia siku zote za mkutano huo kuongeza tija kwenye shughuli zao za Uvuvi na Ukuzaji Viumbe maji.
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu