Na Jackline Martin, TimesMajira Online
BENKI ya Azania wamesaini mkataba na Chama kilele Cha wakulima wadogo wa chai Tanzania lengo ni kuhakikisha mkulima anapata ahueni ya uzalishaji wa majani mabichi ya chai.
Wakulima hao watakatwa shilingi 100 ya Majani mabichi watakayoyauza ambayo itaenda kuwekwa kwenye akaunti maalumu Dunduliza ambayo Benki ya Azania Benki anakua mtunza fedha wao.
Akizungumza na waandishi wa Habari Jana Jijini Dar es Salaam,
Mkuu wa Kitengo Cha Kilimo katika Benki ya Azania, Augustino Matutu alisema wanachokifanya ni muendelezo wa jitihada za serikali za kuwainua wakulima, kuongeza tija na kufikia ajenda kubwa yenye lengo la kunyanyua uzalishaji ulipo sasa mpaka kufikia asilimia 10 kwa mwaka kufikia mwaka 2030
“Malengo haya hayawezi kutimia kama hakuna rasilimali pesa, na rasilimali pesa inapatikana kwa njia mbalimbali ambapo Moja wapo ni njia hii ya wakulima kujiwekea akiba kupitia akaunti ya dunduliza ambapo Benki ya Azania inakua mtunza ela wao, mshauri wao wa mambo ya fedha na pale itakapohitajika tutatoa mikopo”
Alisema wamebaini kuwepo kwa changamoto zinazowakabili wakulima wa wadogo wa chai ikiwemo upatikanaji wa pembejeo ambazo haziji kwa wakati na wakati mwingine wakulima hao kukosa fedha za kuagizia pembejeo hizo.
“Tumeshiriki katika kampeni za Kilimo cha chai ili kujifunza changamoto walizonazo wakulima wa zao hilo, kuangalia fursa nyingi kubwa walizonazo kwenye maeneo yao ya uzalishaji ambapo tumejionea kuwepo kwa changamoto nyingi za upatikanaji wa pembejeo ambazo haziji kwa wakati na wakati mwingine wanakosa fedha za kuagizia pembejeo”
Pia alisema kupitia Dunduliza akaunti ambayo ni maalumu kwaajili ya wakulima wadogo wa chai, Benki yao watachagiza na mabenki mengine kuanza kutoa fedha kwenye Sekta hiyo ya chai.
Kwa upande wake Afisa mkuu Mipango na uhamasishaji Bodi ya chai, Godlove myinga alisema kutokana na wazalishaji wa chai kukosa pembejeo, Bodi ya chai iliwahamasisha wakulima kujiwekea akiba kwa muda Fulani ili kuendeleza Sekta ya chai kwa kuweza kuongeza tija na ubora wa chai
“Ubora wa chai ukiongezeka utasaidia kupata soko zuri, serikali imefanya jitihada kubwa sana ya kutafuta masoko kwa kufungua mnada wa chai dar es salaam, ambao umeanza mwaka Jana Novemba na bado serikali Inajitahidi kuendelea kutafuta masoko mengine “
“Ili upate soko zuri la chai lazima uwe na chai Bora hivyo tunaamini pembejeo hizi zitasaidia sana kuboresha uzalishaji na kuongeza tija na ubora”
Myinga aliwashukuru wakulima hao wa tasnia ya chai na kuiomba Benki ya Azania kuwa mkataba huo uwe endelevu.
Naye Mwenyekiti wa Chama Cha kilele Cha Wakulima wadogo wa chai Tanzania, ,Edwin mahunda alisema nafuu ya uzalishaji wa majani mabichi ya chai, itasaidia kupatikana kwa mbolea kwa kuagiza mbolea kwa pamoja, kupata miche bora ya chai, kupata viua magugu kwenye chai na viwanda vidogo vya bei ndogo vitakavyoziwezesha AMCOS kujitegemea na kujiendesha wenyewe.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa