Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bi.Mwamini Malemi, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 52 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa NSSF. Bi. Malemi alisisitiza uboreshaji wa huduma bora kwa wanachama, kuendelea kuwajengea uwezo wafanyakazi, kuongeza kasi ya ukuaji wa Mfuko kwa kuifikia sekta binafsi na sekta isiyo rasmi na kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika utendaji kazi.
Pia alisema NSSF itaendelea kusimamia maono ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhakikisha kuwa Watanzania waliopo katika sekta binafsi na sekta isiyo rasmi wanasajiliwa na Mfuko, waajiri kuwasilisha michango stahiki ya wafanyakazi wao kwa wakati.
Lengo la mkutano huo ni kupitia Mpango wa mwaka ujao na Bajeti kwa mwaka 2024/25, ikiwa ni ushirikishwaji wa wafanyakazi katika maamuzi ya kiutendaji. Ufunguzi wa mkutano huo umefanyika tarehe 9 Mei 2024 katika Hoteli ya Malaika Jijini Mwanza.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba, akitoa maelezo ya awali kabla ya ufunguzi wa Mkutano wa 52 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi uliofanyika jijini Mwanza. Mkutano huo ulifunguliwa na Bi.Mwamini Malemi, ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya NSSF.
Mkurugenzi wa Usimamizi wa Rasilimali Watu na Utawala wa NSSF, Ekwabi Mujungu, alipata fursa ya kutoa salamu katika mkutano wa 52 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi la NSSF. Mujungu amesisitiza kwa wafanyakazi kuzingatia maadili ya Utumishi wa Umma.
Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma wa NSSF, Lulu Mengele akiratibu ufunguzi wa Mkutano wa 52 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa NSSF, uliofanyika katika Hoteli ya Malaika Jijini Mwanza
Meneja wa NSSF Mkoa wa Mwanza Emmanuel Kahensa akitoa neno la ukaribisho katika jiji la miamba wakati wa Mkutano wa 52 wa Baraza kuu la wafanyakazi wa NSSF
Meneja wa NSSF Mkoa wa Kinondoni Large Materu akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Wajumbe wa Mkutano wa 52 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa NSSF
More Stories
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â