Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
MKUU wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, amesema mwenge wa UHURU mwaka 2024 unatarajia kuwasili wilayani Ilala , siku ya Jumatano Mei 8 mwaka huu ambapo utapokelewa Uwanja wa Ndege wa Teminal One asubuhi, mara baada kuwasili wilayani ILALA utakimbizwa katika miradi ya maendeleo.
Akizungumza live kwa njia ya Simu na Wananchi wa Buguruni Mnyamani alisema mapokezi ya Mwenge wa UHURU unatarajia kupokelewa majira ya saa moja asubuhi na Mkuu wa mkoa Dar es Salaam Albert John Chalamila ,kisha kutukabidhi Wilaya ya Ilala tayari kwa kuanza mbio zake.
“Siku ya Mei 8 tunatarajia kupokea Mwenge wa UHURU nitumie fursa hii kuwaomba Wananchi wangu wa Wilaya ya Ilala na maeneo ya jirani kujitokeza kwa wingi katika Uwanja Ndege kwa ajili ya mapokezi
hayo ambapo Burudani mbali mbali zitakuwepo ikiwemo vikundi vya Hamasa kutoka wilayani Ilala alisema Mpogolo.
Aidha Mkuu wa wilaya Edward Mpogolo alisema Mwenge wa UHURU unatarajia kuzindua miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo kituo cha Polisi Mzinga Mwanagati , Kituo cha afya Kinyerezi na Bangulo Mradi wa maji.
Mpogolo alisema mara baada kukimbizwa katika miradi ya maendeleo Mwenge wa UHURU utalala katika viwanja vya Mnazi Mmoja ambapo alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi wa Ilala kujitokeza kwa wingi katika mkesha huo Burudani mbali mbali zitakuwepo wakiwemo wasanii wa Kizazi kipya na Singeli .
Alisema ujumbe wa Mwenge mwaka huu kauli mbiu yake inasema Tunza mazingira na Shiriki Uchaguzi Serikali za mitaa kwa ujenzi wa Taifa endelevu.
More Stories
Maghorofa Kariakoo mikononi mwa Tume
ITA chatakiwa kutoa mafunzo ya viwango vya juu na kasi ya maendeleo ya Kisayansi
Wagombea CHADEMA wakipewa ridhaa,watakuwa wawazi