January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tulia Trust yarejesha tabasamu kwa Mama mwenye watoto sita aliyetelekezwa na Mume wake

Na Esther Macha, TimesmajiraOnline, Mbeya

TAASISI ya Tulia Trust inayoongozwa Rais umoja wa Mabunge duniani na Spika wa Bunge na Mbunge jimbo la Mbeya mjini Dkt. Tulia Ackson imeendelea kuwajengea nyumba wananchi wanaoishi katika mazingira magumu Jijini Mbeya kwa kuanza ujenzi wa nyumba ya Mama mwenye watoto sita aliyetekelezwa na mume wake aitwaye ,Eliza Mwaifwani mkazi wa mtaa wa Ilolo kata ya Ruanda Jijini hapa pamoja na kuwarejesha shule watoto waliokuwa wamekatisha masomo baada ya kukosa sare za shule pamoja vifaa vya kujisomea.

Akizungumza kwa niaba ya Taasisi ya Tulia Trust Ofisa habari wa Taasisi hiyo ,Joshua Mwakanolo amesema kuwa hivi karibuni walifika nyumbani kwa Mama Mwaifwani na kuona familia hiyo ikiwa na changamoto nyingi ikiwa ni tofauti na maeneo mengine ya mtaa wa Ilolo ambako Taasisi hiyo ilitembelea wananchi wanaoish katika mazingira magumu .

“Siku kadha zilizopita tulifika nyumbani kwa Eliza Mwaifwani kuja kuona hali halisi ya maisha yake lakini pia tulipita mitaa mingine ndani ya Kata hii ya Ruanda kuja kuwatembelea ndugu zetu wanaoishi katika mazingira magumu baada ya kupita tukakutana familia hii yenye changamoto nyngi baada ya kulitambua hilo tuliwasiliana na uongozi wa Kata na kupewa ushirikiano na tulipopata ushirikiano tuliwasiliana na Mkurugenzi wa Tulia Trust Dkt.Tulia na kumweleza juu ya changamoto waliyoikuta ikiwemo watoto wa Mama huyo kukosa elimu kutokana na mazingira ya familia hiyo na baadaye tulifanya mawasiliona na uongozi wa Kata ukiongozwa ofisa elimu kata na kuona jinsi gani watoto wanaweza kuanza masomo kwasababu umri wao bado ni mdogo ,lakini pia changamoto nyingine ikaja kuonekanani ukosefu wa sare za shule na sisi tukahiidi kuwa tutaleta vifaa vyote vya shule pamoja na Madaftari ili waweze kuanza masomo “amesema Mwakanolo

Akielezea kuhusu ujenzi wa nyumba Ofisa Habari huyo amesema kuwa ujenzi huo unaanza leo April 22,2024 na wanategemea uwe umekamilika ifikapo May mwaka huu na kuwa May 11 itakuwa siku ya kilele cha mbio za Tulia Marathon mwaka huu ambapo Dkt. Tulia Ackson ambaye ni Mkurugenzi wa hiyo ya Tulia Trust atakabidhi nyumba hiyo kwa familia ya Eliza Mwaifwani.

Aidha Mwakanolo ameomba uongozi wa kata hiyo kutoa ushirikiano kwa mafundi ambao watakuwa wakijenga nyumba hiyo pindi watakapohitaji nguvu kazi ya kusaidia kazi hiyo ili nyumba hiy iweze kukamilika mapema na familia hiyo iweze kutabasamu kama ambavyo familia zingine zinaishi maisha ya kutabasamu,pia amesema katika nyumba zizojengwa na Tulia Trust kwa wahitaji ni nyumba 11 kwa mkoa mzima wa Mbeya lakini kwa jiji la mbeya itakuwa ni nyumba tisa ambapo leo April 22 ,wameanza ujenzi wa nyumba ya Mama Eliza Mwaifwani lakini Kata ya Iziwa kuna kunma mwitaji mwingine ambaye anajengewa nyumba .

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Ilolo Kata Ruanda ,Ezekiel Mwasandube alimshukuru Spika wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini na Rais Umoja wa mabunge duniani Dktr. Tulia Ackson amesema kuwa kitendo kilichofanywa na Dkt.Tulia ni kitu kizuri na kuwa mchakato huo ulianza wakati familia hiyo ilipopata na msiba wa mtoto mchanga ambapo kifo cha mtoto huyo kilileta picha nyingine ya mazingira ya familia ya Mwaifwani .

Eliza Mwaifwani ni mama mwenye watoto sita amemshukuru Dkt. Tulia kwa kumuona kutokana na maisha magumu aliyokuwa akiishi na familia yake kiasi cha kukatisha masomo kutokana na ukosefu wa sare za shule na vifaa vya kujisomea ambapo iliwalazimu kuacha masomo .

“Mimi nilikuwa nafanya kazi za kufua nguo kwenye nyumba za watu fedha ambayo ilikuwa ikitosha kulisha watoto tu lakini vifaa vya shule vilinishinda na baba wa watoto hajulikani alipo hivyo nimekuwa nikiishi na wanangu kwa kuomba kwa majirani kufua nguo na kupata fedha kidogo ambayo ilinifanya kusaidia kulisha watoto wangu sita ingawa kwa upande wa kununua vifaa vya shule na sare nilishindwa ikabidi watoto waache masomo”amesema Mwaifwani.

Diwani wa Kata ya Ruanda Jijini Mbeya ,Reuben Kipalule amesema kuwa kwa vitu anavyofanya Dkt. Tulia vya kujitoa kusaidia wahitaji amewataka wananchi kuendelea kumwombea ili aweze kuendelea kufanya kazi zake vizuri za kuhudumia wananchi na kwamba kuna viongozi wa upande wa pili walikuwa viongozi lakini hawakudiliki kufanya yote haya yanayofanywa na Dkt. Tulia lakini bado pia ameweza kugusa sekta ya elimu kwa kuwagusa watoto wanaoishi katika mazingira magumu kwa kata 36 za Jiji la Mbeya kwa kuwapatia sare za shule,viatu,Mabegi,pamoja na Madaftari .

“Ndugu zangu tusimpoteze Dkt .Tulia huyu ni lulu kwetu 2025 ipo jirani naomba tusikubali kurubuniwa hii nyumba inayojengwa mtaa wa huu wa Ilolo itatustaki ndugu zangu hatujawahi pata kiongozi kama huyu anayejali wahitaji huyu mama kabla ya kufikiwa na taasisi ya Tulia Trust amekuwa akiishi maisha magumu ambayo yalipelekea watoto kuacha shule kwa ukosefu was are za shule na vifaa vya kujisomea “amesema Diwani huyo.