October 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kamishna mstaafu wa Jeshi la Polisi nchini,Suleiman Kova akikata utepe wakati wa ugawaji wa vifaa vya kunawia kwa wafanyabiashara wanawake wa Soko la Tabata jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Penina Malundo).

Kova: Nina nguvu ya kuendelea kuwatumikia Watanzania

Na Penina Malundo,TimesMajira,Online

KAMISHNA mstaafu wa Jeshi la Polisi nchini, Suleiman Kova amesema licha ya kuwa amestaafu, lakini bado anauhitaji wa kuendelea kuwatumikia Watanzania.

Akizungumzia leo jijini Dar es Salaam katika Mkutano wa Mtandao wa Nguvu ya Pamoja ya Wanawake ( Women Tapo) Kova amesema, licha ya kustaafu, lakini bado anaendelea kufanya kazi na watanzania katika nyanja mbalimbali.

“Nimestaafu bado nawapenda watanzania wenzangu, bado nataka niwatumikie na ndio maana nimeanzishaa taasisi yangu ambayo inanifanya niwe karibu na watanzania wenzangu,”amesema.

Mwenyekiti wa Women Tapo,Stella Mbaga amesema kutokana na wanawake kuwa na mchango mkubwa katika jamii wameamua kuwaletea vifaa vya kunawa mikono katika kupambana na maambukizi ya ugonjwa wa corona.

“Msaada huu tumepata kutoka katika Mfuko wa Wanawake, hivyo tukasema tuwaletee ili nanyi muendelee kujikinga na corona hapa sokoni (Soko la Tabata),”amesema.